Mwandishi wetu,
Babati. Watuhumiwa wa ujangili katika eneo la ikolojia ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Manyara sasa wataanza kusakwa kupitia Mfumo maalum wa kidigitali unaotumika katika kukusanya taarifa,zikiwepo picha, kuzihifadhi na kuzituma(SMART) kwa usahihi.
Mfumo huo wa kisasa utaanza kutumika mwaka huu, katika eneo la jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori Burunge,kupitia mradi wa uhifadhi maliasili unaodhaminiwa na shirika la msaada la kimataifa la Marekani(USAID).
Akizungumza wakati akitoa mafunzo jinsi ya utumiaji wa mfumo, huo kwa askari wa wanyamapori wa Burunge WMA, askari wa halmashauri ya Babati na askari wa Mamlaka ya usimamizi wanyamapori(TAWA)Macarios Gisberth alisema mfumo huo utarahisha kuwadhibiti majangili kabla ya kuuwa wanyapori.
“huu mfumo huu pia utawezesha kufanyika doria katika hifadhi za wanyamapori na kupata taarifa matukio ya ujangili kabla haujatendekeka,matukio ya uvamizi wa mifugo na uharibifu wea mazingira”alisema .
Afisa miradi wa tuhifadhi mazingira, ambao unaendeshwa na taasisi ya chemchem katika eneo la Burunge WMA, Martin Mng’on’go alisema katika mradi huo askari wanaofanyakazi katika eneo hilo, watakuwa wakitumia mfumo huo kukabiliana na ujangili,.
“askari tayari wamejengewa uwezo kufanya doria kutumia mfumo wa SMART , kuwachunguza majangili na kuwakamata kirahisi zaidi”alisema
Afisa wa doria wa Mamlaka ya usimamizi wanyamapori(TAWA),Gabriel Charles alisema mfumo huo wa kisasa ni suluhu jinsi ya kukabiliana na majangili.
“tumeona jinsi mfumo huu, utarahisha upangaji mzuri wa doria, kukusanya taarifa za uhalifu na kuzifanyia kazi”alisema
Afisa Wanyamapori wilaya ya Babati,Godluck Kalambani alisema mfumo huo utasaidia uchakataji wa taarifa na utoaji taarifa sahihi ikiwepo eneo ambalo mtumuhima ataonekana na hivyo kukamatwa kabla ya kutenda uhalifu.
Baadhi wa wahitimu wa mafunzo haya, Janet Gerald askari wa burunge WMA alisema mafunzo waliyopata yamekuwa na faida kubwa kwani sasa watatumia mfumo wa SMART kukabiliana na ujangili.
“tumefundishwa jinsi ya kutumia mfumo huu kupanga doria, kubainisha uvamizi eneo la hifadhi na kubaini eneo alipo jangili kwa urahisi”alisema.
Katika eneo la Burunge WMA kumeibuka matukio ya ujangili wa Twiga mnyama wanyama ambao wapo wengi katika eneo hilo.
MWISHO.