Site icon A24TV News

MBUNGE AIDA AITAKA SERIKALI IJE NA NJIA YA MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZWA KUTIBIWA BILA MALIPO.

Na Doreen Aloyce Dodoma.

MBUNGE wa Jimbo la Nkasi Kaskazini Aida Khenani ameiomba Serikali kuja na njia mbadala ya kusaidia Kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza kutibiwa bila malipo kuelekea kuhitimisha kwa bajeti ya Wizara ya afya Kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Mbunge huyo ameyasema hayo katika viwanja vya Bunge alipokuwa akizungumza katika kuelekea kupitishwa kwa bajeti ya afya kwani afya ndio Kila kitu katika maisha.

Mbunge Aida amesema kuwa Serikali ikiondoa Kodi ya matibabu katika magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile kisukari,Kansa,kifafa pamoja na ajari itasaidia kuokoa maisha ya watanzania wengi.

Amesema kuwa kwa magonjwa yasiyoyaluambukiza ghalama ni kubwa na ngumu kwa mtanzania wa kawaida kuweza kumudu kulipa matibabu hayo.

“Yapo magonjwa ambayo yanaweza kumtokea mtu yoyote mfano ajali inaweza kukumba hata ukiwa nyumbani inaweza kupata ajali,suala la ajali ni lazima Serikali ilitazame kwa kina kwani kunaajali ambazo ni muhimu Ione namna ya kuweza kuwasaidia watanzania,”amesema Mbunge huyo.

Katika hatua nyingine amemtaka waziri wa Afya Ummy Mwalimu kuweka wazi ugonjwa wa Corona kutokana na maneno ya chinichini yaliyopo mtaani .

” Juzi nimefanya utafiti wangu Binafsi nimeenda Duka moja la dawa nimekutana na wananchi kibao wanaulizia dawa ya Corona jambo limeleta mashaka kwa nini serikali haifunguki tujue hali ilivyo huko mahospitalini “alihoji mbunge Khenani.

Mwisho