Site icon A24TV News

MBUNGE JIMBO LA BIHARALO MHANDISI CHIWELESA ALIA NA SERIKALI MAZAO YA KAHAWA, MGOMBA NA TUMBAKU.

Na Doreen Aloyce, Dodoma

Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mhandisi Ezra Chiwelesa ameiomba Serikali kuongeza dhamani ya mazao ya Kahawa aina ya robista , mgomba pamoja na Tumbaku ambazo uzalishwa ndani ya Mkoa wa Kagera.

Kauli hiyo ameitoa Bungeni Dodoma wakati alipokuwa akichangia Bajeti wizara ya Kilimo kwa mwaka 2023/2024 iliyowasilishwa na Waziri mwenye Dhamana Hussein Bashe.

Mhandisi Chiwelesa alizungumzia suala la Miche ya kahawa kuwa imekuwa sintofahamu ya kupewa miche michache licha ya kwamba inazalishwa na wakazi wa kagera ukilinganisha na gharama ya uzalishaji inayotumika jambo ambalo sio sahihi.

“Tunampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kunyanyua kilimo cha nchi hii ambapo kwa sisi Biharamulo kwa mara ya kwanza tunaenda kujengewa mradi wa umwagiliaji(Schem Irrigation ).

“Nikuombe waziri Bashe rudini maabara kuepuka magonjwa ya kahawa na migomba ambayo imeshambuliwa na magonjwa ya mnyauko na kufanya hivyo itasaidia kagera kurudi kwenye hadhi yake. “Amesema Mhandisi Chiwelesa

Aidha amemuomba Waziri kusimamia vyema suala la tumbaku ya Biharamulo inunuliwe ndani na sio kupelekwa nje na kwamba bado kuna tatizo la mbolea ambayo haina ubora inayozalishwa moja ya kiwanda hapa nchini ambayo imepelekea wananchi kupata hasara na kuumia licha ya kwamba wameilipia.

“Tunaomba mbolea isongezwe karibu kwani wapo wananchi waliopo vijijini kikiwemo kijiji cha Kalenge wanasafiri kilometa sabini wanaoshindwa kufika mjini hiyo itawasaidia wananchi kutokuhangaika na usumbufu wa pesa wanaoupata wanapofata mbolea mjini.”

Amesema wananchi kuwa wanamatarajio ya kusikia kauli ya serikali juu ya mwenendo mbovu uliopigiwa kelele wa kiwanda hicho ambacho kinatoa mbolea feki na kurudisha maendeleo nyuma.

Mwisho.