Site icon A24TV News

MBUNGE MWAKAMO KIBAHA VIJIJINI SERIKALI BORESHENI BIMA YA AFYA KWA WOTE.

Na Doreen Aloyce ,Dodoma

Mbunge wa Jimbo la Kibaha vijijini. Michael Mwakamo amesema licha ya serikali kuendelea kuboresha huduma za afya hapa nchini kuna haja ya kuweka mikakati ya kuweka Bima ya afya kwa wote jambo ambalo litasaidia wananchi kupata matibabu kwa urahisi.

Kauli hiyo ameitoa Viwanja vya Bunge jijini Dodoma wakati alipokuwa akifanya mahojiano na waandishi wa Habari juu ya Bajeti ya afya ambayo imepitishwa kwa mwaka 2023/2024.

“Tunaona kazi ya vituo vya afya ilivyo kubwa ujenzi wa zahanati vijijini, namna ya usambazaji wa vifaa vya kutolea huduma za afya zinakwenda mpaka ngazi za chini hii inaleta matumaini makubwa lakini niombe serikali ikazie suala la Bima kwa wote ili wananchi wapate huduma stahiki”Mwakamo.

” Utoaji wa vifaa tiba kwenye maeneo ya vijijini kunarahisha pia kupunguza ongezeko kubwa la mama wanaojifungulia majumbani na vifo vya uzazi vinapungua “amesema mbunge Mwakamo

Aidha amesema ndani ya jimbo lake bado kuna changamoto ya kukosekana kwa madawa kwenye vituo vya afya jambo ambalo serikali wanalitengenezea ya kuwa na bima ya afya kwa wote .

Ametoa wito kwa watanzania kutoa ushirikiano kwa Rais Samia Suluhu Hassani ili zile juhudi alizonazo aweze kufanya mengi huku akiwataka wananchi wa jimbo lake kuendelea kumuunga harakati za kuwapambania na hatawaangusha.

“Niko karibu na wananchi wangu wa kibaha vijijini nawaahidi sitawaangusha nipo Bungeni kuwapambania kumalizia zile changamoto ndogo ndogo zilizopo hususani barabara na maji.” Amesema Mbunge Mwakamo

Mwisho