Site icon A24TV News

MPANGO MAKAMU RAIS TOENI MIKOPO KWA WANCHI YENYE RIBA NAFUU WAWEZE KUFIKIA MALENGO

Na Geofrey Stephen Arusha
Mapema leo akifungua mkutano wa senima kwa wana hisa Makamu wa Rais , Dkt Philip Mpango  amezitaka Taasisi za  fedha na mabenki nchini  kutoa mikopo ya riba nafuu kwa makundi maalum na  mbalimbali wakiwemo wachimbaji wadogo wa madini,wavuvi, wakulima na wafugaji  ili waweze kupiga hatua kujenga uchumi wa taifa. 
 Ameyasema hayo leo jijini Arusha wakati akifungua  mkutano kwa wanahisa wa benki ya CRDB unaofanyika katika ukumbi wa mkutano wa Aicc jijini Arusha.
Alisema kuwa,taasisi n noyingi za fedha zimekuwa zikitoa mikopo ya riba kwa asilimia 9 ,hivyo aliomba kupunguza zaidi chini ya asilimia 9 ili kuwapa fursa wafanyabiashara wadogo na wananchi waliopo vijijini kuweza kupata huduma za mikopo yenye riba nafuu 
Makamu wa Rais  ameyaomba mabenki kuongeza bidii katika kupeleka huduma za kibenki vijijini ili kuwapa fursa wananchi waliopo eneo hilo kupata huduma hiyo kwani hivi sasa ni asilimia 8.6 ya wananchi waishio  vijijini wanaopata  huduma za kibenki hapa nchini. 
 “Baadhi ya mabenki yanakopesha kwa asilimia 9 hivyo yanapaswa kupunguza zaidi ili kuwapa fursa wananchi wa kipato cha chini hasa vijana na wanawake kuweza kukopa  na kujikwamua  kiuchumi”.
Aidha ameyataka  mabenki kubuni madirisha maalumu  ya mikopo  kwa vijana na wanawake ambayo ni sehemu kubwa ya nguvu kazi ya Taifa lakini bado huchukuliwa kama soko gumu kwa huduma za fedha .
 Ataivyo ameyataka  mabenki  kuzingatia ufanisi katika utendaji kazi  ikiwemo kuongeza  gharama za uendeshaji katika matumizi ya Tehama , sambamba  
na kuhakikisha hakuna mikopo chechefu mipya na kuzingatia ukomo  wa asilimia 5 uliowekwa na benki kuu ya BOT.
Naye Mwenyekiti  wa bodi ya benki ya CRDB, Dkt Ally Laay ameomba serikali kupitia wizara ya elimu kuandaa mitaala maalumu ya kuwafundisha wanafunzi umuhimu  wa kuwekeza  katika Hisa ili kuwapa elimu ya fedha wakiwa na umri mdogo.

Aidha ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuwekeza kwenye hisa kwani Hadi sasa Taifa lina mwako mdogo sana ya uwekezaji katika maswala ya Hisa .

 “Bado kuna ufahamu mdogo kwa jamii katika maswala ya Hisa na uwekezaji WA fedha , pendekezo letu  ni kuwa  tuna haja ya kufundisha  somo  la mitaala kwenye shule zetu  ili vijana wapate ufahamu wakiwa wadogo  jambo ambalo litaleta  fikra  chanya  katika uwekezaji wa maswala ya Hisa.”amesema.
Mkurugenzi  wa benki ya CRDB, Abdulmajjid Nsekela alisema kuwa utaratibu waliojiwekea WA kila  mwaka kutoa semina kwa wanahisa umeingeza hamasa  kwa wananchi kununua hisa katika Benki hiyo.

Alisema idadi ya wanahisa  hapa nchini waliojiunga na mabenki ni chache kwa mabenki mbalimbali kutokana na kutokuwa na elimu ya fedha ndio maana kumekuwa  na utaratibu  wa kutumia semina ya wanahisa.

“Watanzania  tupo zaidi ya milioni 60 lakini ukiangalia kwenye mabenki yote nchini wateja hawazidi  milioni 10  wenye akaunti na hiyo ni  kutokana na elimu ndogo ya fedha ndio maana benki hii imeamua kufanya maboresho ya kuwa na semina ya wanahisa jambo lililosaidia  kuongeza  idadi ya wateja wa  benki hiyo”alisema.
Alisema wanahisa WA Benki hiyo wanatarajia kunufaika na gawio Nono la asilimia 45 kwa kila hisa tofauti na mwaka jana lilikuwa ni asilimia 35 na hiyo ni baada ya Benki hiyo kupata faida ya sh,bilioni 365 baada ya Kodi.
Mwisho .