Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limemfikisha mahakamani mtuhumiwa Isaack Mnyangi (45)Mkazi wa Sombetini Jijini Arusha na kusomewa shtaka moja la shambulio la Kudhulu Mwili.
Mbele ya Hakimu ,Jenifa Edward wa mahakama ya wilaya Arusha,katika kesi namba 80 ya mwaka 2023,mwendesha mashtaka wa serikali ,Charles Kagilwa akisaidiana na Godfrey Nungu na Callorine Kasubi,alidai  mnamo Mei 23 mwaka huu majira ya saa tano usiku katika eneo la Osunyai kwa Diwani jijini Arusha
 
Mshtakiwa Mnyangi alimshambulia Jackline Mkonyi(38)ambaye ni mke wake na kumng’oa jino moja ,kumpiga kwa Mkanda Usoni na mgongoni na maeneo mengine ya mwili wake na kumsababishia madhara.


Hata hivyo mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo na upande wa jamhuri ulidai upelelezi wa shauri hilo umekamilika na kuiomba mahakama kumsomea mshatakiwa maelezo ya awali .
 
Akisoma maelezo kwa mshtakiwa, wakili wa jamhuri Godfrey Nungu alidai mnamo Mei 23 mwaka 2023,majira ya saa tano usiku ,mhanga(Jackline)alisikia mlio wa honi ya gari nje ya geti na alipojaribu kwenda kufungua  alibaini kuwa mtoto wake wa kiume tayari alikuwa ameshafika getini kufungua
 
Wakili Kagilwa alieleza mahakama kuwa Mhanga aliendelea kumsubiria Mhuhumiwa sebuleni lakini mtuhumiwa alipoingia ndani hakumsalimia badala yake alipitiliza chumbani .


Alidai kuwa Mhanga alimfuata chumbani lakini mhuhumiwa alimshika mkono na kumvuta  na kusha kumtupa Sebuleni kwenye Kochi .
 
Alieleza kuwa Mtuhumiwa alianza kumpiga Mhanga kwa ngumi Usoni na kuendelea kumpiga mateke na kumkanyaga na baadaye alichomoa mkanda wake wa suruwali na kuendelea kumpiga katika meneo mbalimbali ya mwili wake ikiwemo mgongoni.
 
Alidai kwamba mtuhumiwa alichukua Plaizi na kumng’oa jino moja la mbele, ambapo mhanga alitokwa na damu nyingi akiwa hajitambui.


Wakili aliendelea kudai kuwa, mhuhumiwa alimwacha Mhanga akiwa na majeraha makubwa mwilini akiwa anavuja damu nyingi hapo sebuleni na kwenda kuwaamsha watoto na baadaye alimpigia simu mama yake na Mhanga(mama mkwe)na kumweleza kuwa anamleta mtoto wake nyumbani. 
 
Alieleza kuwa mhanga huyo alipakia kwenye gari pamoja na watoto na kwenda hadi Sinoni Daraja mbili nyumbani kwa mama mkwe na kumtelekeza na kutoweka kusikojulikana .
 
Alidai kwamba siku iliyofuata Mhanga alipelekwa hospitali na kushondwa majeraja na daktari alithibitisha kuwa Mhanga alikuwa amng’oa jino moja na kutobolewa sehemu ya jicho lake. 
 
Alidai uchunguzi wa polisi ulifanyika na mtuhumiwa alikamatwa mei 27 mwaka huu akiwa amejificha kwa mchungaji eneo la Himo Mkoani Kilimanjaro na baadaye kufikishwa mahakamani.
 
Hata hivyo upande wa jamhuri ulidai kuwa utakuwa na mashahidi watano na kielelezo kimoja.
 
Hata hivyo upande wa jamhuri uliwasilisha maombi madogo ya kupinga dhamana kw mshtakiwa na kueleza mbalimbali ikiwemo, mshtakiwa kutoroka baada ya tukio,hali ya taharuki kwa wananchi pamoja na kujenga chuki kwa mkewe na watoto.
 
Hakimu aliahirisha shauri hilo kwa saa moja na baadaye mahakama ilirejea na kutoa maambuzi ya kukubaliana na ombi la upande wa jamhuri la kumnyima mshtakiwa dhamana kwa siku 14 hadi juni 13 mwala huu ambapo mahakama  itatoa masharti ya dhamana.
 
Mshtakiwa alipelekwa  rumande katika gereza kuu la Kisongo,Arusha hadi juni 13 mwaka huu.
 
Ends….