Na Geofrey Stephen Arusha.
Kadinali wa pili wa kanisa la Ngurumo ya upako linaloongozwa na Nabii Mkuu Mh Dkt Geordavie jijini Arusha, Elizaberth Humphrey amemshukuru MUNGU kwa jambo kubwa lililofanyika tarehe 28 Mwezi May 2023 katika kanisa hilo kwa kumpa tuzo Nabii mkuu Dkt GeorDavie.
Amesema tangu walipofika Ngurumo ya Upako kwa Nabii Mkuu GeorDavie mahali amefanyika kuwa baraka Kubwa sana kwao kwasababubu amekuwa mtu mwenye matendo yenye kugusa mioyo ya watu wengi.
Amesema kuwa amekuwa Baba Mwema kwa watu wote bila kujali kabila wala Dini ndio maana watoto wake mbele za MUNGU kwetu sisi wote.
Amesema alitutoa kwenye matatizo mengi ikiwemo kuanguka kiuchumi lakini kila tulipomsogelea kwa upako ambao MUNGU ameweka ndani yake na yale mafuta ya kimungu tunazidi kufunguliwa na kuwa huru”,amesema Elizabert.
Ameongeza kuwa hiyo ndiyo sababu imewafanya kuwa na sherehe ya kumtunza Baba yao wa kiroho Mhe, Nabii mkuu Dkt. GeorDavie balozi wa Amani.
Amesema kuwa hiyo tuzo imetengenezwa Nchini China na imetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu sana kama mnavyoona muonekano wake ndani yake ina Moyo wa Dhahabu safi pia ina ishara ya tufe maana yake Dunia nzima inatambua umuhimu wake na gharama yake imeharimu kiasi cha fedha za kitanzania sh milioni kumi.
kwa upande wake Balozi wa Nabii Mkuu Sekela Ntondolo amesema siku ya tuzo iyo imekuwa siku nzuri sana kwao kwasababu walikuwa wanamkabidhi Baba yao wa kiroho Nabiii mkuu Dkt GeorDavie tuzo ya heshima .
Amesema wamefanya kwasababubu ya kutambua umuhimu wake hivyo wasingeweza kuona anapewa tuzo na watu wengine ambapo wao wamejisikia fahari sana kwakuonyesha kwamba Nabiii Mkuu Mh Dkt GeorD1avie anafanya kazi kubwa anayoifanya kwenye maisha yao.
Sekela amesema kuwa wengi walifika hapo Ngurumo ya Upako wakiwa wamefungwa kichumi na nguvu za giza maisha ni mabaya na hukuna tumaini mahali popote lakini zaidi ya hilo walifunguliwa katika vifungo hivyo napia amewabariki.
Amesema mfano yeye mwenyewe ni mubarikiwa ambaye ameweza kubarikiwa magari kwahiyo baba yao ni mtu ambaye anagusa maisha ya watu kiroho na kimwili na nyie ni mashahidi jinsi ambavyo anawabariki watu wengi kiuchumi pikipiki za miguu mitatu (Bajaji) mitaji magari na heshima.
Ameongeza kuwa Nabii Mkuu amekuwa ni mtumishi wa tofauti kabisa na ameleta sura mpya kwa kanisa la Tanzania kwa kupitia hilo ndilo lililopelekea na sisi kutambua kazi yake na kuweza kumpa tuzo ya heshima tunasikia furaha sana kupokea tuzo yetu.
Mwisho .