Site icon A24TV News

Serikali yashauriwa kutumia kiswahili kwa maslahi ya nchi. “Mbunge Haji”

Na Doreen Aloyce, Dodoma

Mbunge wa Jimbo la Pangawe Haji Amri Haji amesema kuwa ili Taifa liweze kusonga mbele kiuchumi kunapaswa kuwa na lugha ya kiswahili huku akiitaka Sekta ya Elimu kubadilka katika ufundishaji wa lugha .

Mbunge Haji ametoa kauli hiyo Katika Viwanja vya Bunge wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari juu ya Bajeti ya Elimu kwa mwaka 2023/2024 ambayo imepitishwa na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha amesema kuwa nchi nyingi za ulaya zilizoendelea hususani nchi ya Lashia na China zimekuwa zikitumia lugha zao kwa sababu ya mfumo wa kibiashara na mfumo wa kiuchumi na hiyo imepelekea kuwa na mafanikio makubwa .

“Ninachotaka kumanisha ni kwamba tunapaswa kwa sisi Tanzania tunapaswa kubadilika katika ufundishaji wa Lugha tunapaswa kuchanganya lugha mbili ya kiuchumi na lugha ya Ufaulu ambapo katika ufaulu mtu anaweza kujifunza lugha kwa namna yoyote”

 

” Mimi binafsi nina mawazo kwamba ili nchi iweze kuendelea tunapaswa kuwa na lugha mama ya kiswahili na kama tunataka lugha ya ufaulu tungechanganya lucha zote sio kiingereza tu hata kifaransa na lugha nyunginezo” amesema Mbunge Haji.

MWISHO.