Site icon A24TV News

TTCL YAPONGEZWA KUFIKISHA MAWASILIANO KILELE MLIMA KILIMANJARO. “Dkt. TULIA

Doreen Aloyce, Dodoma

SERIKALI imesema Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) licha ya kufanya vizuri limeendelea kujipambanua katika utoaji wa huduma zake za Mawasiliano iliyopelekea kufikisha huduma za mawasiliano Kilele cha Mlima Kilimanjaro.

 

Hayo yamebainishwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson wakati alipotembelea na Kukagua Banda la Shirika hilo lililopo katika Maonesho yaliyoandalaliwa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ,kwa taasisi zilizopo Chini yake yanayoendelea katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.

Dkt.Tulia amesema kuwa TTCL mbali na ubunifu wao wamekuwa chachu kuifungua nchi kidijitali jambo ambalo limesaidia kuchochea maendeleo ya Mtu mmoja mmoja na taifa Kwa ujumla.

“Niwapongeze sana shirika kwa kazi nzuri mmekuwa mfano bora kwa Taifa ,Mmeifungua nchi Kimawasiliano ukweli huo lazima tuusema Kwanza hili la kupeleka huduma ya Mawasiliano katika Kilele cha Mlima Kilimanjaro ni jambo la kupongezwa Kwa nguvu zote Kwani sasa Kila mmoja anaweza kuwasiliana na ndugu na jamaa wakiwa hata huko huko kileleni haya ni maendeleo, “amesema Dkt.Tulia

Aidha Dkt.Tulia amezungumzia pia huduma zinazotolewa na Shirika hilo za Majumbani ikiwemo huduma ya Fiber Nyumbani Kwako na Smart home kuwa zinasaidia kurahisisha Mawasiliano na kusimamia ulinzi na Usalama.

kwa upande wake Meneja wa Biashara wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Jijini Dodoma Leyla Pongwe, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Shirika hilo,amesema kuwa Kasi ya Shirika hilo katika kuleta mapinduzi ya Kimawasiliano ni kutaka kuhakikisha agenda ya Serikali inafanikiwa ya kutaka kufikia Uchumi wa Kidijitali ifikapo 2025.

“Serikali ina malengo ya kuhakikisha uchumi wa kidijitali unakuwa kwa kasi ifikapo 2025 sasa Jukumu letu kama Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL ni kufungua njia kuhakikisha malengo hayo yanafikiwa,”amesema

Amesema TTCL imekuja na huduma Mpya yenye malengo ya kurahisisha upatikanaji wa huduma ya Mawasiliano na Usalama Kwa mtumiaji wa huduma hiyo

Pia Leyla amesema ili kuhakikisha ulinzi na Usalama Majumbani Shirika hilo wamekuja na huduma ya Smart Home ambapo mtumiaji atakuwa ana uwezo wa kufuatilia mambo yote yanayoendelea Nyumbani kwake hata kama yeye hayupo Nyumbani kupitia Application hiyo inamuwezesha kujua Kila kitu kinachoendelea Nyumbani kwake.

Hivyo Mtumiaji akiwa na huduma ya Fiber Nyumbani Kwako na Smart Home anakuwa na uhakika wa Mawasiliano na Usalama wa Mali zake hata kama hayupo Nyumbani.

Pia amesema kuwa Kwa sasa Shirika hilo linajipanga kuhakikisha wanafikisha huduma ya Fiber katika nchi za jirani kupitia Mkongo wa Taifa ambao Kwa sasa huduma ya Mawasiliano imefika Kila Mpaka unaoizunguka Tanzania.

Hata hivyo amesema wana Kituo Cha kuhifadhiTaarifa “DATA CENTER” ambapo Kituo hicho kinasaidia kuhifadhi taarifa na data za mtumiaji, mtoa huduma na hata taarifa za serikali zinaweza kuhifadhiwa kupitia Kituo hiki na zinakuwa salama .

Mwisho.