Na Doreen Aloyce, Dodoma
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wamiliki wa Kampuni ya ASASI inayozalisha maziwa kuendelea kuhudumia jamii hususani kuzalisha maziwa kwa wingi na yenye ubora.
Kauli hiyo ameitoa katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma wakati alipokuwa akitembelea maonyesho ya wafugaji na wavuvi kwa ajili ya kuonyesha protini yaliyoandaliwa na Wizara ya Mifugo na uvuvi .
Waziri Mkuu ametumia nafasi hiyo kuwapongeza Kampuni hiyo ya ASAS na kuwataka waendelee kuhudumia jamii kwa kuzalisha maziwa mengi na Bora na kuyasafirishwa ndani na nje ya nchi.
Aidha amemuagiza Waziri wa Mifugo na uvuvi kuwa kampuni kama ASAS na nyinginezo waangalie namna ya kuweza kuzisaidia kwani zinafanya kazi kubwa ya kuzalisha bidhaa ambazo zinaweza kuuzika hata nje ya Nchi.
“Wizara imeonyesha mikakati wa namna inavoboresha sekta ya Mifugo na uvuvi,namna Serikali inayoongozwa na Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kutenga fedha ya kutosha kwa sekta mbili na tumeweza kupata mafanikio na tumeona changamoto zilizojitokeza huko nyuma,
Tukiwa tunaendelea na mawasilisho yetu ipo fursa ya wabunge kuchangia kwa sekta hizi mbili za Mifugo na uvuvi kwa kuchangia maoni ya wananchi wanavyoeleza na pia wanatoa muelekeo wa Nini Wizara ifanye,”amesema Waziri Mkuu.
Kwa upand
“watanzania tumepiga hatua kwani Mifugo na uvuvi ni utajiri unaweza kuinua Pato la Nchi na uchumi wa mtu mmoja mmoja,
Tunakila sababu ya kujivunia hili na kuendelea kuongeza kasi katika kuitunza Mifugo yetu ili tuendeleze kuzalisha Mifugo mingi na Bora zaidi,”amesema.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ASAS Fuad Asas amesema Wizara ya Mifugo na uvuvi imewapa ushirikiano hasa katika kusaidia uzalishaji wa maziwa na upatikanaji wa ng’ombe Bora kwa kuwaunganisha na wafugaji wa ng’ombe Bora.
Kadhalika alisema kuwa ipo haja ya Wizara ya Mifugo kuhakikisha inatoa elimu ya kutosha kwa wafugaji ili kuepusha matatizo yatokanayo na maziwa kutoka kwa ng’ombe kwenda Kwa mlaji.
Balozi wa ASAS Lucas Mhuvile alimaarufu JOTI
amesama kuwa lengo kuu ni kuhakikisha jamii kwa ujumla inapata elimu ikiwa sambamba na kutumia maziwa kwa wingi ili kuimarisha na kuboresha afya zao.
Maonyesho hayo yamehudhuriwa na wabunge mbalimbali kwa lengo lankujifunza na kujionea bidhaa zinazozalishwa kutokana na mifugo .
Mwisho.