Site icon A24TV News

YANGA YAONYESHA UKUBWA NUSU FAINALI YAICHAPA TIMU YA MARUMO MBILI BILA .

Na Mwanamichezo wa A24Tv .

Timu pekee ya wananchi Yanga African leo kwa mkapa imefanikiwa kulamba kitita cha Shilingi Million 20 za Mh Rais wa Jamuhuri wa Muungano Samia Sulubu Assan mara baada ya kujiweka nafasi nzuri ya kutinga Fainali ya Michuano hiyo baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Marumo Gallants ya nchini Afrika Kusini katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa  nusu fainali uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Kipindi cha kwanza timu zote zilikuwa zikishambualiana kwa zamu na kupekeleka kwenda mapumziko zikiwa hazijafungana.

Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko hata hivyo Yanga SC walinufaika na mabadiliko hayo mnamo dakika ya 64 Stephane Aziz Ki alianza kuitanguliza Yanga Sc mbele baada ya kufunga bao zuri akipokea pasi kutoka kwa Tusila Kisinda

Akitokea benchi kiungo Mtukutu Benard Morrison alipigilia msumari wa pili katika dakika za jioni kabisa

Pamoja na ushindi huo kocha wa yanga amesema kwamba  Tumeshinda lakini sijaridhishwa na kiwango cha wachezaji wangu.”