Site icon A24TV News

BABA ASKOFU MKUU WA KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI RIKI DK.MBILU ASHIRIKI MBIO ZA MWENGE WILAYANI LUSHOTO (M) TANGA

Na *Mwl.Mohamed Mwampogwa* -LUSHOTO TANGA_
____________________________________

_Yapo baadhi ya mambo huonekana niya kawaida unapo yasikia au kuyaona yametendeka mahala fulani lakini katika uhalisia kwa wahusika waliofanya matukio hayo na Jamii yao hubaki kama jambo lenye maajabu na kugusa Historia ya maisha yao._

_Hili limetokea katika Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Wilayani Lushoto kwa kuweka historia kwani Baba Askofu mkuu Dr.Mbilu wa kkkt dayosisi ya kazkazini Mashariki ashiriki mbio za Mwenge wa Uhuru 2023._

_”Haikuwahi kutokea kuona Kiongozi kama huyu Dk.Mbilu kuweza kushiriki kukimbiza Mwenge,iliamsha hisia za Upendo,mwenyewe nilihisi Roho wa Mungu wetu yupo pamoja nasi,tunawashukuru Viongozi wetu wa Chama na Serikali yetu kwa kuyashirikisha makundi yote katika Jamii bila ubaguzi kwenye shughuli za kitaifa na ujenzi wa taifa” Alisema Mama Alice Shemdoe._

_Mwenge wa Uhuru Wilayani Lushoto huwa kama Sherehe za kitaifa na Wananchi hufanya maandalizi ya kuupokea tena mara unapo maliza mzuunguko wake ndani ya Wilaya.Miradi yote ya maendeleo katika Halmashauri mbili za Wilaya ya Lushoto na Majimbo matatu ya Lushoto,Bumbuli na Mlalo yamewekewa Jiwe la Msingi.Huku Mkuu wa Wilaya Mhe.Kalisti Lazaro Bukhay akiwashukuru Wana Lushoto na Wadau wote wa maendeleo walio shiriki katika kufanikisha zoezi la mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2023._
____________________________________