Site icon A24TV News

DED KAHAMA AMSHUKURU RAIS KWA KUMUAMINI

Na Richard Mrusha kahama

MKURUGENZI wa Manispaa ya Kahama ,Mkoani shinyanga Anderson Msumba amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa kuendelea kumwamini na kumuacha aendelee kuiwakilisha vyema Serikali Kwa kuwatumikia wananchi wa Manispaa hiyo.

Amesema anamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan Kwa kumuamini na kuendelea kumuacha kwenye kituo chake cha Kahama ili aiendelee kumuwakilisha kuendelea kuwatumikia wananchi Kwa kutatua kero mbalimbali ndani ya Manispaa hiyo.

Msumba ameyasema hayo wilayani humo Juni 14 ofisni kwake katika mahojiano maalumu na waandishi wa Habari juu ya maendeleo ya Manispaa hiyo ambapo Amesema kuwa ataendelea kufanya kazi Kwa weredi ili kuweza kusonga mbele katika kuwaletea maendeleo wananchi .

” Wenye sifa wapo wengi na wanafaa kuwa wakurugenzi lakini kwa Imani yake Rais Dkt Samia kwangu amendelea kunipa nafasi na Mimi nahaidi stomwangusha nitaendelea kuchapa kazi ili kuleta matokeo chanya Kwa wananchi wetu.”Amesema mkurugenzi Msumba

Ameongeza kuwa kazi kubwa ya Halmashauri ni ustawi wa wananchi wake huku akisema kuwa Manispaa hiyo ni kubwa sana na inaendelea kukua kwa haraka Kila kukicha hivyo kutokana na hali hiyo changamoto zinakuwa ni nyingi lakini amefarijika kubaki Kahama ili yeye pamoja na timu yake watimize ndoto yao ya kuiona Kahama mpya yenye maendeleo makubwa na ya Kasi ya ajabu.

“Mimi Nimefarijika nimebaki Kahama angalau Mimi na wenzengu tunataka kuona zile ndoto zinatimia, na kubwa zaidi kuifanya kahama kuwa kitovu cha biashara “amesema Msumba.

Nakuongeza kuwa ” Naiona kahama kwenda kuwa kama Dubai na kupitia uwekezaji mkubwa utakaofanyika pale bandari ya Dar es Salaam niwazi biashara katika mji wa kahama itakuwa kubwa.

Aidha katika hatua nyingine Mkurugenzi Msumba amesema kuwa kwa sasa wamewekeza nguvu kubwa kwenye miundombinu ya Elimu, Afya na Kwa kiasi furani waendelea kufanya vyema nakwamba kama Manispaa wamejipanga vilivyo.

“Bado kuna shida sana kwenye eneo la Fursa watu wetu waweze kufanya shughuli za kiuchumi na niseme sisi kama Kahama tangu 2017 kupitia Mpango wetu mkakati wa miaka mitano mitano, tunataka kuona Kahama iwe eneo kubwa la biashara kama mnavyojua kwamba Kahama ni njia kuu kwenye maziwa makuu Kwa maana ya Rwanda, Burundi, Drc Congo,na Uganda.

Amesema kuwa nchi hizo zote zinatumia bandari ya Dar es salaam na kahama pia ni mji ambao unahudumia mikoa ya Kigoma,Geita, Tabora, Kagera Kibiashara hivyo ndio maana amesema kupitia uwekezaji unaokwenda kufanyika katika bandari ya Dar es salaam utaongeza fursa katika mji wa kahama .

Awali Amesema Manispaa hiyo ya Kahama imetenga maeneo makubwa ya uwekezaji na Viwanda na mpaka Sasa Kuna ekari elfu sita(6000) Kuna ekari 2000 Nyashimbi na eneo jingine ni eneo la Mgodi wa Buzwagi ambalo linamilikwa na PANGEA pamoja na maeneo mengine ya uwekezaji kama Zongomela eneo la Viwanda na kwingineko..

Mwisho.