Site icon A24TV News

JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAKABIDHIWA MAGARI 8 NA BALOZI WA NCHINI NCHINA YENYE GARAMA YA DOLA 400,000

Na Geofrey Stephen Arusha .

SERIKALI ya watu wa China imetoa Msaada wa magari 8 yenye thamani dola 400,000 pamoja na vipuri vyake kwa jumuiya ya Afrika Mashariki( EAC) .

Aidha pamoja nakuleta wataalamu wa kutoa mafunzo ya matumizi ya magari hayo kwa madereva na mafundi wa Jumuiya ya nchi za Afrika mashariki kwa ajili ya kuboresha shughuli za EAC.

Akiongea mara baada ya kukabidhi magari hayo Balozi wa China nchini Tanzania CHEN MINJUAN kwenye makao makuu ya EAC Jijini Arusha amesema kwamba zoezi hilo lilikuwa lifanyike mwaka 2021 lakini kutokana na janga la uviko ndio maana limefanyika mwaka huu.

Amesema serikali ya watu wa China imekuwa ikishirikiana na nchi za jumuiya ya Afrika mashariki katika masuala mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa miundombinu mbali mbali sanjari na kusaidia kukuza Demokrasia uwajibikaji na utawala bora.

“Tumekuwa tunasaidia katika nyanja mbalimbali kwa lengo la kukuza Amani Demokrasia Utawala Bora na uwajibikaji utakaosaidia jamii ya watu wa Afrika Mashariki kupata huduma bora”

Kwa upande wake mwakilishi wa Katibu mkuu EAC na Mkurugenzi wa sekta ya maendeleo ya Jamii, Irene Isaka amesema kwamba Jumuiya ya Afrika mashariki imekuwa ikishirikiana na serikali ya watu wa chini katika masuala mbalimbali ya kijamii katika kukuza mtangamano.

Alisema kwamba magari hayo yatasaidia shughuli mbali mbali za Kijamii katika mataifa 7 ya EAC ikiwemo matamasha ya vijana na wajasiriamali na sio kwa ajli ya ubebaji na shughuli za wa wafanyakazi wa jumuiya pekee.

Mwisho .