Site icon A24TV News

MBUNGE MSTAAFU MR 2 ,SUGU AWAFUNDA WANAFUNZI WA VYUO NILISHAWAI KUA MLINZI NILIPATA UBUNGE KWA KUBEZWA SANA , NINA HOTEL KUBWA YA KITALII

Na Geofrey Stephen Arusha.

Wito umetolewa kwa serikali kutengeneza mazingira mazuri ya kuwasaidia vijana wanaomaliza katika vyuo mbalimbali hapa nchini ili waweze kujiajiri ikiwa ni pamoja na kusimamia Sera za vijana zilizopo na kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.

Akizungumza katika Semina kubwa ya kuwajengea vijana namna ya kugikia nfoto za kua  wajasiriamali kutoka katika vyuo mbalimbali ujulikanao kwajina la UNIVERSITY ENTREPRENEUR SUMMIT uliofanyika jijini Arusha na kuwahusisha wanafunzi wa vyuo mbalimbali vilivyopo jijini Arusha Mkurugenzi wa Chuo cha Help Self Help kilichopo jijini Arusha .

Amani Golugwa amesema serikali ina wajibu wa kusimamia Sera za vijana zilizopo ili kuwasaidia kujiajiri pindi wanapomaliza katika vyuo Na kuingia katika somo la ajira .

Amesema lengo la mkutano huo ni kuhamasisha vijana kuwa na ujasiri na uthubutu wa kutumia vipaji walivyo navyo ili kujiajiri wenyewe na kuweza kusukuma maisha bila kutegemea kupata ajira serikalini.

Kwa upande wake aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Mjini ambaye pia alikua  mgeni rasmi katika Semina iyo Joseph Mbilinyi almaarufu kama Mr.2 Sugu amesema kuwa ili kijana aweze kufanikiwa lazima awe na ndoto atakayo isimamia kuelekea mafanikio yake.

Wakati akizungumza na wanafunzi hao Sugu amewataka wanafunzi kueshu kile wanacho amini atakama ni biashara ya Mihogo wafanye kwa kumaanisha kwani biashara yoyote ni uwaminifu na luga  njema pamoja na kujituma na kusimamia ndoto .

awali alieleza kwamba kabla ya kufikia mafanikio yale alianza kufanya kazi ya ulinzi kwa miaka minhi na baadae alivyo pata pesa alikimbilia muziki nako alipata mafanikio makubwa na kujikuta akingia kwenye siasa.

aliwaambia wanafunzi hao wakati anagombea ubunge watu walimbeza kwamba msanii wa muziki awezi kua mbunge kwani kazi ya muziki ni huuni jambo ambalo alipambana kuuza sera na akashinda ubunge kwa awamu mbili na sasa ni mwekezaji mkubwa katika biashara ya hotel mjini mbeya

Nae mkuu wa chuo cha Help Self help Elizabeth Benedict amesema kuwa masomo ya fani huibua wazo la ujasiriamali na usimamizi wa biashara huku mwezeshaji wa Jimy Pamba akieleza kuwa vijana wengi wanaotoka vyuoni hawazalishi bidhaa kulingana na elimu zao .

Amesema mwanafuzi anapofika chuoni hapo anapata mafunzo ya kujikita kujisimamia kua wabunifu wenye uwezo wa kujiamni kufanya kazi popote pale wanapo kwenda kufanya mazoezi ya fani walizo somea jambo ambalo wanajivunia toka kuanzishwa kwa chuo hicho kumekua na mapokeo makubwa kwa wanafunzi wanao ondoka chuoni hapo .

Baadhi ya wanafunzi washiriki wameeleza manufaa waliyo yapata kupitia mafunzo yaliyofanyika katika Semina hiyo na kueleza kwamba wamepata kitu cha kipekee ambacho kimewajenga na kupata uzoefu wa kusimamia ndoto zao na kufikia malengo katika kutatua chagamoto za ajira nchini .

Wanafunzi hao wameomba mafunzo ayo kua endelevu chuoni hapo kwani yana tija kubwa sana na yanalenga kuwajengea uwezo wa kutambua namna ya kujisimamia katika kuanzisha biashara au kufungua makampuni na namna ha kusimamia taasisi .

Mwisho.