Site icon A24TV News

Mgodi wa Dhahabu Handeni Wafungwa Serikali yakosa Mapato kisa Mabroka Mwekezaji atumia mamilioni ya pesa kuwezeka

Na Geofrey Stephen Handeni

Afisa Mfawidhi wa Madini Mkoa wa Tanga,Zabibu Napacho amesitisha shughuli za Uchimbaji katika mgodi wa Dhahabu ulipo katika kijiji cha Kwandege Kata ya Lang’ata Wilayani Handeni Mkoani Tanga unaomilikiwa na Godfrey Bitesigirwe  kutokana na mgogoro uliopo  baina ya mmiliki wa mgodi huo na wenye maduara na kwani kunaweza kuhatarisha Usalama na Amani katika eneo husika.

Napacho alisitisha shughuli za uchimbaji juni 6 mwaka huu katika mgodi wa dhahabu wenye lesseni ya uchimbaji mdogo na uchenjuaji madini –PML 0330-0337TNG-Kwandege na kusema kuwa agizo hilo ni maagizo ya Mkuu wa Wilaya ya Handeni ,Albert Msando.

Kamati ya ulinzi  na usalama ikiwa eneo la mgodi wakipata maelezo namna uchimbaji unavyo fanyika 

Alisema agizo hiloni  kufuatia kikao cha pamoja kati ya Mkuu wa wilaya pamoja na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo ,viongozi wa chama na serikali na mmiliki wa mgodi huo katika kikao kilichofanyika juni 6 mwaka huu katika shule ya msingi Kilimazinga.

Afisa Madini Zabibu Napacho 

Afisa Madini huyo alisema kuwa agizo hilo limetolewa kutokana na mgogoro uliopo kati ya Bitesigirwe na wenye lesseni zingine katika eneo hilo lengo ni kutoa nafasi ya kufanyika kwa hatua za mbalimbali zitakazopelekea kutatuliwa kwa mgogoro huo kwa utulivu na amani.

‘’Aidha Mkuu wa Wilaya ya Handeni ameagiza kusitishwa kwa shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa Madini kwenye lesseni zako PML0330-0337TNG zilizopo eneo la  Kwandege Kijiji cha Kilimamzinga’’alisema nakala ya Afisa Madini

Hata hivyo Bitesigirwe alionyesha kutokukubali agizo hilo na kutoa sababu nane za kupinga agizo hilo ikiwa ni pamoja na kuzuia kwake kuendesha shughuli za uchimbaji zinatoa mwanya kwa uchimbaji usio rasmi kuendelea katika mgodi wake na hauna tija kwa pande tatu yenye mwenyewe,Serikali kuu,Halmashauri na Tume ya Madini kwani dhahabu inayopatikana hutoroshwa na kuuzwa kusikojulikana na kuitia hasara serikali.

Bitesigirwe alisema kuwa alinunuwa mashine kubwa na za kisasa za uchimbaji na uchenjuaji zenye gharama kubwa na kuaminika katika benki ya NBC na kukopeshwa m,amilioni ya pesa hivyo hutakiwa kufanya marejesho kila mwezi lakini kutokana na hali hiyo huenda akashindwa kufanya hivyo na wachimbaji wadogo wadogo kushindwa kuaminika katika benki.

Katika picha ni wachimbaji wakiwa wanasikiliza kwa umakini viongozi waliofika katika eneo la uchimbaji wa dhaabu 

Alisema yeye hana mgogoro wowote na wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu katika kijiji cha kwandege bali kuna madalali wa dhahabu{Broker’s} wanaosafiri kwenye migodi ya dhahabu Nchi ndio wanaochochea mgogoro huo na kutoa taarifa za uongo kwa viongozi wa juu wa serikali hatua ambayo haileti afya kwa wakazi wa Handeni.

Mwekezaji huyo mzawa alisema yeye anamiliki leseni nane katika eneo la Kijiji cha Kwandege alizopewa mwaka 2019 kwa kufuata taratibu zote za Tume ya Madini na alianza uchimbaji mwaka 2020 na katika muda wote hakuwahi kuwa na ugomvi na Kijiji,wachimbaji wengine wala viongozi wa chama na serikali ngazi ya wilaya hatua ambayo anashindwa kujua ni sababu zipi zimepelekea yeye kusitishiwa shughuli za uchimbaji kwani sababu zilizoelezwa yeye anaziona hazina mashiko.

Alisema kuwa toka ameanza uchimbaji amekuwa na ushirikiano mkubwa na wamiliki wengine wa lesseni nne na pia amekuwa akitumia mamilioni ya fedha kwa huduma za jamii kama vile ujenzi wa zahanati,utengenezaji wa madawati na milango,ametoa msaada wa nondo na simenti na upanuzi na ukarabati wa barabara  ya kutoka Kilimamzinga hadi Kijijini kwandege.

Akizungumzioa tukio hilo,Mkuu wa Wilaya ya Handeni,Albert Msando alikiri kumwagiza Afisa Madini kusitisha shughuli za uchimbaji dhahabu katika lesseni hiyo na kusema kuwa hiyo ni kutokana na wahusika kupewa muda mwingi kukaa chini na kutafuta suluhisho lakini ilishindikana.

Msando alisema yeye kama Mwenyekiti wa Ulinzi wa Usalama wa Wilaya ya Handeni hataki kuona mgogoro wowote ndani ya Wilaya hiyo hususani katika machimbo ya dhahabu kwani amani iikitoweka viongozi wa juu watamuuliza yeye sio mtu mwingine yoyote.

Alisema na kuwataka wachimbaji wa dhahabu Handeni wenye lesseni na wasiokuwa na lesseni kufuata taratibu pindi kunapotokea mgogoro katika migodi wanayochimba ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha viongozi wa serikali ngazi ya kijiji,kata,wilaya na Mkoa kwa kufanya hivyo kunaweza kutatua changamoto zilizopo bila kuangalia sura wala kabila.

Mwisho.