Site icon A24TV News

MILLIONI ZAIDI YA 200 KUPATIKANA HARAMBEE YA UJENZI WA KITUO CHA AFYA SEPEKO”

Na juliana Laizer

Kufuatia Ujenzi wa kituo Cha Afya kilichoanza tangu 2020 kusimama bila kutokana na ukosefu wa Mapato katika vijiji vya kata hiyo ,hatimaye Suluhu lapatikana baada yakufanyika harambee katika kata hiyo.

Harambee hiyo imehusisha vijiji vinne vinavyounda Kata ya Sepeko, ikiwemo Kijiji mama Mtimmoja, Lendikinya, Arkatan, na Arkaria Ambapo Kila Kijiji kilitoa shilingi millioni 10.

Akiongoza Harambee hiyo Mbunge WA Jimbo la Monduli Fredrick Lowassa kwa niaba ya Mgeni Rasmi Mh Waziri wa Madini Doto Biteko amewataka wananchi kuendelea kuwa na Imani na Serikali ya Awamu ya sita katika Maendeleo Ambapo kati ya millioni 248 zilizopatika zaidi ya 100m zimetoka kwake kwa kushirikiana na wadau wake , Huku zaidi ya Million 20 zikitokana na wadau/Marafiki wa Diwani Kimaai wa kata hiyo.

Aidha kwa Upande Mwingine Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Mh Issack Kadogo Amesema kupitia Mapato ya ndani Halmashauri itatoa millioni 50 , huku akitupa lawana kwa viongozi wa Kata hiyo , kufuatia kukwama kwa ujenzi kisa Ukosefu wa mapato kwani hawajawahi kutoa Taarifa yoyote kwake , huku binafsi akitoa Matofali Elfu Moja (1).

Viongozi Mbalimbali walishiriki katika Harambee hiyo Akiwemo Mbunge mstaafu Ambaye kwa Sasa ni DC Karagwe mh Julius Kalanga , Jeshi la Wananchi Lililozunguka kata hiyo kwa pande zote, Mwanzilishi wa Shule ya msingi na Sekondari Khatimul Aambiya Mzee Gulamu ,Wafanyabiashara wa kata hiyo, Wazee wa Mila ,Vijana ,na Kinamama,pamoja na wengine ndani na nje ya Wilaya hiyo.

Sambamba na Hilo Diwani wa kata hiyo Diwani Kimaai Amesema lengo la kuhitaji kituo Cha Afya katika kata hiyo ni kutokana na wingi wa watu, Taasisi mbalimbali zilizopo , zikiwemo shule za Sekondari ambazo zote ni za Bweni wenye watu zaidi ya elfu 25, vijiji 4, na kusema endapo kituo hicho kikikamilika Kitahudumia pia Kata za Jirani ikiwemo Makuyuni na Lepurko.