Site icon A24TV News

MWENGE WA UHURU WAZINDUA DARAJA LA KISASA LA MLESA.DULE M. WILAYANI LUSHOTO

Na Geofrey Stephen

Lushoto Tanga Matukio katika picha likionyesha uzinduzi wa daraja la kisasa la mlesa  kata ya Dule M wilayani lushoto ambapo Mwenge wa Uhuru Kitaifa ulizindua mradi huo mkubwa wa garama ya shilingi Milioni 270,892 ,140.00 fedha zinazotokana na tozo ya mafuta .

Mradio huu umeanza kutekelezwa mnamo tarehe 02 mwezi wa 11,2022 ambapo ulitarajiwa kukamilika ambapo  kwa sasa mradi upo kwenye kipindi mtazamio .

Aidha katika utekelezaji wa  mradi huo makundi mbali mbali ya wananchi walipata fursa ya kunufaika kwa kupata ajira za muda pia mradi baada ya kukamilika umefanikisha kuondoa adha ya usafirishaji iliyo dumu kwa muda mrefu katika kata tatu za  Mwangoi Dule na Rangwi na kuongeza mzunguko wa fedha baada ya kuboreshwa kwa miundo mbinu hiyo .

Ataivyo wakala wa Barabara za vijijini Tarura wamemshukuru Mh Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzanaia Mh Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Fedha za mradi huo na miradi mingine na kuaidi kuzisimamia Fedha hizo kutekeleza yenye  ubora zaidi .

Mwisho .