Site icon A24TV News

NAIBU WAZIRI WA MADINI DKT KIRUSWA AMALIZA MGOGORO NA KUFUNGUA MGODI WA DHAHABU HANDENI ONYO KALI WANAOTOROSHA MADINI

Na Geofrety Stephen Handeni Tanga

Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ameufungua mgodi wa Dhahabu unaomilikiwa na Mwekezaji Mzawa Godfrey Bitesigirwe uliopo  Kijiji cha Kilimamzinga kata ya Kang’ata Wilayani Handeni Mkoani Tanga na kuwataka wachimbaji wote wa Dhahabu kuheshimu mipaka ya leseniya mwenye mgodi vinginevyo watachukuliwa hatua.

Mbali ya hilo pia Waziri Kiruswa ametoa onyo kwa  wachimbaji wadogo wadogo wa Madini ya Dhahabu kuacha mara moja tabia ya kutorosha madini hayo kwa njia ya panya bila kulipa ushuru wa serikali na kusema kuwa serikali haitawaacha salama pindi watakapokamatwa.

Dkt Stephen Kiruswa akizungumza na wachimbaji hao 

Dkt. Kiruswa alisema hayo katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Kilimamzinga mara baada ya kutembelea mgodi huo na kupata maelezo kwa mwekezaji mzawa anayemiliki leseni nane za uchimbaji dhahabu na kusikiliza kero za wachimbaji wadogo wadogo ,Mwekezaji mzawa na viongozi wa Kijiji na Kata.

Baada ya kuwasikiliza,Kiruswa alitoa maagizo kwa wafanyabiashara wasio na leseni kushirikiana na mwekezaji katika shughuli za uchimbaji pia alimwagiza mwekezaji poto{mdomo wa kuingilia mgodini}ili kuondoa changamoto ya kuwa na mashimbo mengi yenye kuharibifu wa mazingira na kuepusha mianya ya utororoshaji.

Dkt Kiruswa alitoa onyo kwa askari polisi waliopewa dhamana ya ulinzi eneo hilo kushiriki utoroshaji wa madini kuacha mara moja tabia hiyo kwani inajenga sifa mbaya kwa jeshi hilo.

Alisema na kuwataka wachimbaji wadogo kufanya shughuli za uchimbaji wa madini katika eneo hilo kwa siku 90 kwa kufuata leseni zao zinavyowaelekeza na anayeshimu maagizo ya Mkuu wa Wilaya ya Handeni Albert Msando ya awali ya kuufunga Mgodi huo.

Akizungumzia utoroshaji wa madini ya Dhahabu, Dkt. Kiruswa ametoa anyo kwa wachimbaji wadogo na wafanyabishara wa madini wanaotorosha madini kwa lengo la kukwepa kodi ya Serikali ambapo amewataka kufuata Sheria na Kanuni zilizowekwa na Serikali ikiwemo kuuza madini katika Masoko na Vituo vya Ununuzi wa Madini vinginevyo hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watoroashaji.

Waziri Kiruswa alitoa muda wa mwezi mmoja kuondoa vibanda vyote vilivyoko katika mgodi huo na kufukia mashimbo ambayo hayatumiki na kuwataka wachimba kupanda miti ili kulinda mazingira.

Alisema serikali itamlinda mwekezaji mwenye kutambulika na serikali kwa gharama zote kwa kuwa analipa kodi ya serikali na serikali itawalinda wachimbaji wadogo wadogo watalindwa na serikali kwa huruma kwa kuwa ni wavamizi katika mgodi huo.

‘’Serikali haina msalimia mtume kwa watoroshaji wa madini ya aina yoyote hivyo basi kwa wale wenye nia ovu dhidi ya madini ya Dhahabu kwa kutaka kujitajirisha haraka haraka na kukwepa kodi ya serikali rungu halitawacha salama’’

‘’Serikali itamlinda mwekezaji wa gharama yoyote kwa kuwa inamtambua kwani ndio tuliompa leseni na kingine analipa kodi kubwa ya serikali’’alisema Kiruswa.

Naye Mbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini John Sallu amempongeza Dkt. Kiruswa kwa kuumaliza mgogoro uliokuwepo katika eneo hilo ili wachimbaji wadogo wadogo wa Dhahabu waweze kunufaika na rasilimali hiyo iliyopo katika kijiji hicho na serikali ngazi zote ziiweze kunufaika na kodi.

Sallu ameiomba Wizara ya Madini kutenga maeneo  kwa ajili ya wachimbaji wadogo hususan maeneo yenye leseni ya utafiti yaliyoisha muda wake ili waweze kufaidika na rasilimali madini zilizopo wilayani humo.

Akizungumza mara baada ya mgodi kufunguliwa Godfrey  ,Bisitegirwe kwanza aliishukuru serikali kwa kufunguliwa mgodi wake na kuahidi kusimamia maelekezo yote yaliyotolewa na serikali ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya mgodi kwa kuweka mdomo mmoja wa kuingilia ndani ya mgodi.

Mwekezaji huyo ambaye kwa sasa ameajiri wafanyakazi zaidi ya 94 ameahidi kutoa ajira kutoana na uzalishaji na kuahidi kuwa na mahusiano mazuri kwa jamii ikiwa ni pamoja na kutoa miaasa pindi anapohitajika kwa faida ya wakazi wa Kijiji kufaidi rasilimali ya madini ya dhahabu.

Alisema atahakikisha anathibiti utoroshaji wa madini ya dhahabu kwa wachimbaji wasiokuwa na leseni wanofanya uchimbaji haramu chini ya mgodi ikiwa ni pamoja na kufukia mashimbo yote ya mtobozano ndani ya mgodi wake kwa wachimbaji hao.

Mwisho