Site icon A24TV News

RUWASA YAKAMILISHA MRADI MKUBWA WA MAJI WA MILION 430 .9 MWENGE WA UHURU WAZINDUA BILA KASORO

Na Geofrey Stephen ,Lushoto Tanga

Watu Zaidi ya 5,621 wa Vijiji viwili vya Kizanda na Mayo vilivyoko katika Halmashauri ya Bumbuli Wilayani Lushoto Mkoani Tanga huenda wakaondokana na adha ya kusaka Maji umbali mrefu baada ya Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini(RUWASA) kukamilisha mradi wa Maji wenye thamani ya shilingi milioni 430.9

Hayo yalisemwa na Meneja wa RUWASA Mkoa wa Tanga, Mhandisi Pendo Lugongo mbele ya kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Abdallah Shaibu Kaimu muda mfupi kabla ya kuuzindua mradi huo.

Lugongo alisema mradi wa Maji katika Vijiji vya Kizanda na Mayo ni miongoni mwa miradi ya Maji iliyokamilika kwa kusimamiwa na kuratibiwa na RUWASA  kupitia fedha za Mpango wa Maendeleo uta Ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko 19.

Alisema mradi huo uliwekwa jiwe la msingi na kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa mwaka jana na ulitekelezwa na Mkandarasi Mbesso Construction ya Jijini Dar es Salaam  hadi kukamilika na unaweza kumtua mama mzigo wa ndoo kichwani na watu Zaidi ya 5,621 watanufaika na mradi huo wa Maji.

“RUWASA tunatoa shukrani za dhati kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutupatia fedha za miradi ya Maendeleo kwani fedha hizo tutazisimamia vizuri ili ziweze kuleta tija kwa Wananchi na kufika malengo yaliyokusudiwa” alisema Lugongo.

Naye Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa, Abdallah Shaibu Kaimu amewapongeza RUWASA kwa kazi nzuri ya kumtua Ndoo mama kwa kuzindua mradi wa Maji na kusema kuwa fedha zilizotumika katika mradi.    huo zimezingatia kikamilifu thamani ya pesa na taratibu za manunuzi kwa mujibu wa Sheria ya   Umma.

Kaimu alisema na kuwataka RUWASA kufanya kila jitihada kuhakikisha huduma ya Maji inasambaa katika Halmashauri yote ya Bumbuli ili kuwwondolea adha akina mama kusafiri umbali mrefu kusaka Maji pasipokuwa na sababu za msingi kwani RUWASA Wana uwezo wa kutatua changamoto ya Maji katika Halmashauri hiyo.

Meneja wa RUWASA Wilaya ya Lushoto,Mhandisi Haron Kizinga alisema kuwa mradi huu una umbali wa km 15 na una vituo 15 vya kuchota hudumaya Maji na RUWASA imeruhusu Wananchi kuunganisha kwenda majumbani na Bodi ya Maji imeshaundwa kwa ajili ya usimamizi wa mradi huo.

Mwisho