Site icon A24TV News

SHUGHULI ZA UCHIMBAJI ZA REJEA KATIKA MGODI WA DHAHABU WA MWEKEZAJI MZAWA GODFREY KAMA MWANZO

Na Mwandishi wa A24Tv.

Siku chache baada ya kufunguliwa kwa mgodi wa dhaabu ulioko kijiji cha kilimamzinga kata ya Kang’ata Wilayani Handeni Mkoani Tanga unao milikiwa na mwekezaji mzawa Godfrey  Bitesigirwe  umeanza kazi za uzalishaji kama hapo awali kabla ya kufungwa.

Mwekezaji wa mgodi wa Dhahabu Godfrey  Bitesigirwe akizungumza na vyombo vya habari kuhusu shughuli zikiendelea katika mgodi wake 

Taarifa zilizo fanywa  na Kituo hiki  zimebaini  kwamba mara baada ya maelekezo ya Mh Naibu Waziri shughuli mbali mbali za uzalishaji za  uchimbaji wa dhaabu unaendelea pamoja na maboresho ya kuweka mazingira vizuri ikiwemo upandaji wa miti pamoja na kuondoa vibanda vilivyo agizwa kuondolea ndani ya mwezi moja kwa lengo la kupisha maboresho ya uchimbaji wa kisasa .

Aizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi Mwekezaji Godfrey Bitesigirwe amesema toka kumefunguliwa kwa mgodi huo shughuli zimerejea kama awali jambo ambapo inawapa kutekeleza maagizo ya Mh Naibu Waziri wa Madini Stephen Kiruswa kutaka mgodi huo kufikia malengo ya kuboresha machimbo yake kama uwongozi ulivyo omba kufanyia maboresho .

Viongozi wa kijiji pamoja na kata wamesema ni faraja kwao kuona shughuli zimerejea kama awali kwani wanapenda kuona jamii ikifanya kazi za mikono na kujipatia vipato kwani wanapo fanya uzalishaji wananufaika na uwekezaji wa kuwepo kwa migodi ya dhaabu katika kijiji na kata hiyo .

Waziri Kiruswa hivi karibuni  akifungua mgodi huo alitoa muda wa mwezi mmoja kuondoa vibanda vyote vilivyoko katika mgodi huo na kufukia mashimbo ambayo hayatumiki na kuwataka wachimba kupanda miti ili kulinda mazingira.

Alisema serikali itamlinda mwekezaji mwenye kutambulika na serikali kwa gharama zote kwa kuwa analipa kodi ya serikali na serikali itawalinda wachimbaji wadogo wadogo watalindwa na serikali kwa huruma kwa kuwa ni wavamizi katika mgodi huo.

‘’Serikali haina msalimia mtume kwa watoroshaji wa madini ya aina yoyote hivyo basi kwa wale wenye nia ovu dhidi ya madini ya Dhahabu kwa kutaka kujitajirisha haraka haraka na kukwepa kodi ya serikali rungu halitawacha salama’’

‘’Serikali itamlinda mwekezaji wa gharama yoyote kwa kuwa inamtambua kwani ndio tuliompa leseni na kingine analipa kodi kubwa ya serikali’’alisema Kiruswa

Mwisho