Site icon A24TV News

BILIONI 7 .282 KUKAMILISHA MIRADI YA MAJI KATIKA ALMA

Na Geofrey Stephen .Arusha

Naibu Waziri wa Maji,Mhandisi Maryprisca Mahundi. amesisitiza wakandarasi waliosaini miradi ya sh, bilioni 7.282 kukamilisha miradi hiyo kwa wakati ili kuwezesha wananchi wapate maji kwa araka zaidi  ikiwemo kuwatua ndoo kichwani wanawake na wananchi kwa ujumla.

Mhandisi Mahundi alimetoa maagizo hayo leo Jijini Arusha kwenye halfa ya utiaji saini mikataba minne ya ujenzi wa miradi ya maji vijijini katika wilaya za Arusha .

Amesema miradi hiyo ni lazima ikamilike kwa wakati na serikali inauwezo wa kutumia wazawa katika kufanikisha hatua mbalimbali za miradi ya maji hususan ya vipuri.

“Tunampongeza Mh Doctar  Samia Suluhu Hassan kwa miradi mikubwa anayofanya ikiwemo suala la bandari lakini tutahakikisha hatumkwamishi tunasambaza maji ili kupeleka maendeleo kwa wananchi”

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella mara baada ya kushughudia utiaji saini mikataba hiyo
amesema serikali ya awamu ya sita inafanya mambo mbalimbali ya kuleta maendeleo Mkoani Arusha na kusisitiza kuwa serikali inasimamia zaidi maslahi mapana ya watanzania.

Miradi hiyo minne yenye thamani ya sh,bilioni 7.282 inatekelezwa maeneo manne ambayo ni mradi wa maji ambapo utekelezaji wa mikataba hiyo itakayohudumia watu zaidi ya 54,000 watanufaika nayo .

Mkandarasi mshauri wa kampuni ya Bene Consult (T)LTD ,Bernard Msaday ameishukuru serikali kwa kuwaamini na kuahidi kuifanya kadri ya utaalam wao ulivyo katika kuhakikisha wananchi wanapata maji huku mwakilishi wa kampuni ya Jandu,Nitu Jandu alisema nafasi walizopewa watazifanyia kazi ili kuhakikisha wanakamilisha kazi kwa wakati

Kwa upande wao wakandari kutoka kampuni ya Climax Unit LTD,Ahamed Kijuu anayetekeleza mradi wa maboresho ya Maji  wilayani Karatu ,  aliishukuru serikali kwa kuwatumia  wakandarasi wazawa katika  kutekeleza miradi hiyo na hivyo kuondoa dhana kwamba wakandarasi wa kigeni pekee ndo wenye uwezo. 

Alisema awali kulikuwa na dhana  kwamba wakandarasi wa ndani hawana uwezo wala vitendea kazi vya kufanya kazi ila anashukuru serikali kwa kuona umuhimu wao na kuwapatia kazi.

 

Kijuu ambaye anatekeleza mradi wa bilioni 1 kwa mkataba  wa mwaka mmoja katika vijiji vya Matala na Endonyawet wilayani Karatu aliahidi kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa na kwa kuzingatia muda ukiopangwa.

Mwisho