Site icon A24TV News

HII NDIO CHUMA ILIYO TOA UHAI WA PADRI MARA BAADA YA KICHAA KUMPIGA ENEO LA KISOGO

Na Geofrey Stephen Karatu.

Paroko wa Kanisa la Katoliki Parokia ya Karatu Jimbo la Mbulu, Mkoani Arusha Pamphili Nada ameuwa kwa kupigwa na chuma ya mlango wa kanisa mara baada ya kuingia Kanisani kwa nguvu kutaka kusali kufanyiwa maungamo baada ya kusema ameteseka kwa muda mrefu na mapepo.

Mara baada ya kuingia kanisani  kichaa huyo aliyejulikana kwa jina la Romani Leonard (30) kufanya mauwaji hayo nae akauawa na Wananchi wenye hasira kali baada ya kengele kulia ya kanisa na waumini kufurika katika kanisa kujua nini kimetokea kanisani hapo .

Waumini wa parokia hiyo mara baada ya kufika kanisani hapo walikuta mwili wa Patri umelala chini huku akimwagika damu maeneo ya kisogoni ambapo walimnyanyua na kumkimbiza hospital kwa lengo la kupata matibabu .

Ataivyo Padri alifariki wakati anapelekwa hospitali na Mtuhumiwa aliuwa na wananchi wenye hasira baada ya kupata taarifa za tukio hilo.

Baadhi ya wakazi wa Karatu walisema Kichaa huyo, tangu usiku wa kuamkia leo alikuwa anataka kuingia Kanisani lakini walinzi walikuwa wanamzuia.

Waumini wa kanisa, hilo walionyesha kusikitika na tukio  hilo la Patri wao kufanyiwa mauwaji majira ya Asubuhi na kichaa huyo .

Mpaka A24Tv inaondoka katika parokia hiyo kamati ya mazishi ikiongozwa na Mwenyekiti wa  halmashauri ya walei Parokia ya  Karatu Mishen Sebastian Antony amesema kwamba wamefikia marehemu kuzikwa Jimboni Mbulu  Mazishi ni siku ya Juma mosi saa saba mchana.

Kamanda wa polisi mkoa Arusha, Justine Masejo amethibitisha kutokea kwa kifo hicho Leo Julai 19,2023 kutokea mauwaji hayo.

Mwisho