Site icon A24TV News

MEYA WA MANISPAA YA MOSHI HOI KWA KIPIGO KIZITO KUTOKA KWA DIWANI! KISA FEDHA ZA MAENDELEO

Na Mwandishi wa A24Tv .Kilimanjaro

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi, Zuber Kidumo amejikuta akichezea kichapo kikali kutoka kwa diwani mwenzake,ABUU SHAYO wakati akiendesha kikao cha kamati Ya Mipango miji na Ardhi katika manispaa hiyo.

Tukio hilo limetokea leo majira ya saa sita mchana wakati kamati hiyo ikiendelea na kikao chake ,ambapo wajumbe wa kamati hiyo walikuwa wakiuliza maswali mbalimbali kwa mstahiki meya huyo ili kupata ufafanuzi wa masuala ambayo wanaona hayako sawa.

Mmoja Ya wajumbe wa kamati hiyo Abuu Shayo ambaye ni diwani wa kata Ya mji Mpya,katika manispaa hiyo,alihoji mchanganuo wa sh,milioni 50 zilizotumika kwenye ujenzi wa madarasa mawili Ya shule Ya msingi ,wakati kunafedha kiasi cha sh,Milioni 20 zilizotolewa na Rais Samia Suhulu na kutosha ujenzi wa darasa pamoja na madawati yake.

Taarifa zimedai kuwa Meya alimjibu kuwa taarifa za ujenzi wa madarasa hayo zitatolewa kwenye kata yake ,hata hivyo diwani huyo alionesha kutoridhika na majibu hayo kwa sababu Meya alimwahidi kumjibu katika kikao hicho.

Diwani huyo hakuishia hapo aliomba kuuliza swali jingine ambapo alihoji matumizi Ya sh,milioni 920 zilizotumika kujenga ukuta unaozunguka Manispaa hiyo usiopigwa hata plasta wakati kuna jengo la Gorofa pamoja na ofisi za watendaji ziligharibu kiasi cha sh,bilioni 1na kudai kuna kuna harufu Ya upigaji kwenye ujenzi wa ukuta.

Swali hilo lilimkasirisha meya huyo ambapo alishuka kutoka kiti cha mbele alikokuwa ameketi na kumfuata diwani huyo aliyekuwa ameketi viti vya wajumbe na kumkwida kwa kumshika tai akidai amezidi kuuliza maswali ya kuchokonoa vitu kila siku.

Lakini Meya huyo alijikuta akiambulia kipigo Kikali kwa kupigwa makofi , mateke na kugaragazwa Chini na kupigwa na chupa za maji na baadaye aliokolewa na walinzi wa Halmashauri hiyo akiwa amelowa chepe .

Askari hao wa manispaa walimwokoa kwa kumtoa nje,huku wakionekana kufurahia kipigo alichokipata,walisikika wakisema “amezidi kiherere .ends