Site icon A24TV News

MGOMO MKUBWA WA DALA DALA !GUTA USAFIRI MPYA ARUSHA BAADA YA DALADALA KUGOMA MADEREVA WA DALADALA WAMTAKA RAIS SAMIA BAJAJI NI KERO MJINI

Na Geofrey Stephen Arusha

Wakazi wa Jiji la Arusha  wameonjañ joto la jiwe mara baada ya madereva wa dala dala kugoma kwa kile wanacho dai kuingiliwa na bajaji kusafirisha abiria katikati ya jiji la Arusha .

Adha ya usafiri imesababishwa na mgomo wa daladala unaoendelea katika barabara zote za Jiji la Arusha na Arumeru kushinikiza kuondolewa kwa bajaji katika ruti zao.

Wakazi wa Jiji la Arusha wakiwa wanasubiria usafiri wa Guta kuelekea katika maeneo ya makazi .

Akizungumzia hali hiyo miongoni mwa abiria, Amina Hassan amesema mgomo huo umeanza leo asubuhi umesababisha mateso makubwa kwa wakazi wa Jiji la Arusha pamoja na wanafunzi wanaotumia usafiri huo kuwahi makazini na shuleni.

“Tunaomba Serikali itafute suluhu ya jambo hili kwani tunaoteseka ni wananchi na hili jambo la daladala kugoma imekuwa siyo mara moja,” amesema.

Ramadhani Ally aliiomba serikali kusikilizwa madai ya daladala na kutatua changamoto hiyo.

“Shida hawa daladala wanataka wao wenyewe ndio wafanye kazi ya usafirishaji wakati hii ni biashara huria, inafaa kila mtu acheze kwenye nafasi yake kupata kipato.

Akizungumzia mgomo huo, Mwenyekiti wa Chama cha Wasafirishaji Mkoa wa Arusha na Kilimanjaro, Locken Adolf amesema kuwa utitiri wa bajaji umeathiri biashara ya daladala hivyo wanaiomba serikali kuzipunguza.

“Ukubwa wa eneo la Arusha, hazitakiwi kuzidi zaidi ya 100 lakini sasa zimekuwa nyingi na zimekuwa kero sana na zimeteka ruti zote za daladala. Pia zinafanya biashara ya kupakia abiria kama wanavyofanya wenzao jambo ambalo siyo makubaliano wakati zinaingia mjini,” amesema.

Amesema kuwa katika ufuatiliaji wamebaini bajaji nyingi ndani ya Jiji la Arusha hazina leseni lakini zinaruhusiwa kufanya kazi tofauti na daladala ambazo zimekuwa zikipigwa faini kila hatua.l

Akizungumzia adha hiyo Ofisa Mfawidhi wa  Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra), Mkoa wa Arusha, Amani Mwakalebela amesema kuwa wamesikia mgomo huo na wanaendelea na taratibu za kushughulika na madai ya madereva hao wa daladala.

 

Mwakalebela amekiri ongezeko la bajaji ndani ya Jiji la Arusha hasa ruti za Sombetini-Ngusero, pia njia ya Majengo, pamoja na ile ya Uswahilini -Dampo ambapo wameanza kuhukua hatua.

“Kweli kuna ongezeko la bajaji ambapo katika 350 zilizosajiliwa na zoezi kufungwa lakini kwa haraka haraka kuna zaidi ya bajaji 2,000 ambazo zinafanya kazi na kugeuka kero, hivyo tulichoamua ni kuomba oda ya mahakama kuzipiga mnada bajaji ambazo tutazikamata hazina usajili wala leseni na uzuri tulishafunga mwaka jana,” amesema Mwakalebela.

Mwisho