Site icon A24TV News

SAKATA LA BANDARI SHEKHE ARUNA USSEN AWATAKA MAWAKILI WALIOFUNGUA KESI WAFUTE MAHAKAMANI

Na Mwandishi wa A24tv .

Msemaji mkuu wa taasisi ya Twariqa Tulikadiriya Jailania Tanzania Shekhe Haruna Hussein amewataka wanasheria ambao wamekwenda mahakamani kupinga suala la Uwekezaji wa Bandari hapana nchini badala yake wakutane na Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ili kuweka sawa Jambo Hilo Kwa maslahi mapana ya Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Arusha shekhe Haruna alisema kwamba kitendo Cha kwenda mahakamani ni kumdhalilisha Amiri Jeshi Mkuu.

“Kila Mwanasiasa ana haki ya kutoa maoni yake lakini kwenda mahakamani sio sahihi badala yake watangulize hofu ya Mungu,na waombe kukutana na Mheshimiwa Raisi na Kwa vile ni msikivu basi wanaweza kuweka sawa.”Alisema Shekhe Haruna

Aidha alisema kuwa serikali ya awamu ya sita imeongeza uwazi katika mambo mbali mbali,ambayo awali yalikuwa hayafanyiki awali hivyo ni vema wananchi wakamuunga mkono Raisi Samia Suluhu Hassan.

“Unajua unapokuwa kiongozi huwezi kufanya mambo ya maendeleo tena magumu alafu mtu akapenda lazima vipingamizi viwepo lakini ni lazima maendeleo yawafikie wananchi.”Alisisitiza Shekhe Haruna

Aliongeza kuwa swala la bandari na Uwekezaji wake linapaswa kuunganisha umoja wa nchi,na sio kuligawa Taifa hivyo amewaomba wanasiasa kutumia fursa yao kuweza kuzungumza na Mheshimiwa Raisi na sio kutoa maoni Yao jukwaani ambao ufumbuzi wake hauwezi kupatikana.

“Nayazungumza haya Kwa ndugu zangu wanasiasa watumie hekima maana hili japo linamhusu Amiri Jeshi Mkuu,sio sawa ndugu zangu tutumie hekima tuombe Kuonana na Raisi na Kisha kutoa maoni yetu hata kama kakosea na Mimi naongea kama kiongozi wa dini sio Mwanasiasa hebu tusaidiane hilo tuweke hofu ya Mungu kwanza.”Alisema Shekhe Haruna

Alisisitiza kuwa kuendelea kunadi mkataba huo mbele ya majukwaa ni kumnyima usingizi na kusababisha kuwa na hofu wakati watanzania tupo zaidi ya milioni 60,hivyo aliomba busara kuendelea kutumika katika jambo Hilo
Mwisho.