Na Geofrey Stephen MIRERANI
Mkuu wa Mkoa wa Manyara,Quen Sendiga amewataka wachimbaji wadogo wa Tanzanite ,waliopo katika katika mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro ,mkoani Manyara, kusaidia kuibua maendeleo katika mkoa huo hususani katika sekta ya elimu ili kuisaidia jamii ya kifugaji kuwapeleka watoto kusoma.
Sendiga ametoa rai hiyo jana wakati alipotembelea shule ya msingi ya Saniniu Laizer yenye mchepuo wa kiingereza katika ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo,ambapo katika shule hiyo ilijengwa na mchimbaji huyo serikali imepeleka sh,milioni 69 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili na matundu ya vyoo
Mkuu huyo wa Mkoa alisema jitihada ya bilionea Laizer zimeisaidia serikali kufikisha elimu iliyobora kwa jamii ya kifugaji na Rais Samia Suluhu hasani amefurahishwa na jambo hilo na alimtuma mkuu huyo wa mkoa kumfikisha salamu zake kwa bilionea Laizer kwa kumweleza kuwa serikali ipo pamoja naye na inaunga mkono jitihada za wadau wa maendeleo .
“Ndugu yetu Laizer ametufanyia jambo kubwa sana TENA la kihistoria, RAIS Samia anaunga MKONO jitihada za wadau wa maendeleo ndio maana ameleta FEDHA kiasi cha sh,milioni 80 katika shule hii ya Laizer”
Alisema mkoa wa Manyara una madini mengi ikiwemo Tanzanite lakini wachimbaji wengi wamekuwa wakivuna na kuondoka na hivyo aliwataka kuona umuhimu kuibua na kuchangia maendeleo kama ambavyo bilionea Laizer amejenga shule na baadaye kuikabidhi serikali.
Kwa upande wake Bilionea Laizer alimshukuru rais Samia kwa kukubali kupokea shule hiyo ambayo ilikuwa ni ndoto yake ili jamii ya kifugaji ambayo ipo nyuma kielimu kuweza kupata elimu ili bora bora.
⁷”Tunamshukuru sana rais samia kwa kukubali kuendeleza shule yetu maana jamii yatu ya kifugaji ipo nyuma sana kielimu”
Laizer aliahidi kuendelea kuchangia maendeleo katika nyanja mbalimbali kwa kutoa sehemu ya mapato yake na kuwataka wadau wengine wa maendeleo kujitoa kadri wanavyopata ili kuiunga mkono serikali.
Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka alimshukuru Mkuu wa mkoa kwa kusimamia miradi yenye thamani kubwa ambayo Rais Samia ametoa fedha nyingi za Maendeleo.
Alisema katika eneo la wafugaji aliiomba serikali kuongeza nguvu katika kuipatia elimu jamii ya kifugaji ikiwemo kuiendeleza shule ya bilionea Laiser ili watu wa jamii hiyo wapate elimu bora na kuachana na chana kurithisha mifugo bali wawarithishe elimu.
Mwisho