Site icon A24TV News

TanaPlay Kuleta Mapinduzi Ya Muziki Tanzania. -Ni Aibu kwa Muimbaji Wa Muziki wa injili kuwa masikini

Na Queen Lema,Dar es salam

Waimbaji wa Muziki wa injili hapa nchini wametakiwa kuzingatia ubora wa kazi zao, ili kuleta ushindani katika tasnia hiyo ya Muziki ndani na nje ya nchi.

Hayo yamesema na Mkurugenzi wa kampuni ya Muziki hapa nchi TanaPlay Mudic Platform Bwana Daniel Mngoma Dcom, wakati akizungumza na A24Tv hili, ofisini kwake Ukonga, Dar es salaam.

Mkurugenzi huyo amebainisha kwamba, sanaa ya Muziki pamoja na huduma kwa Ujumla imekua ikipata changamoto hasa sokoni, kutokana na ubora wa kazi kuwa chini.

“Ninapozungumzia ubora namaanisha kuanzia Audio na kisha Video, Sisi kama TanaPlay tumekuja na suluhisho ambalo naamini Muziki wetu wa injili utakuja kuheshimika zaidi na hatimae waimbaji watajivunia kuitwa katika wito huo” Alisema Dcom

Mbali na hayo ameeleza kuwa, TanaPlay imeanzisha studio za kurekodi Muziki hapa nchini ikiwa ni sehemu ya kuleta mapinduzi katika Muziki wa injili pamoja na kuwaheshimisha waimbaji.

“Waimbaji wetu wengi ni masikini, na wengi wanategemea kuimba ibadani wapewe nauli ndio warndeleze maisha yao, matokeo yake wanadharaulika na wengine wanakata tamaa kabisa, sasa hii sio hali nzuri kwa watu waliopewa zawadi kubwa ya sauti na Mungu, sasa hii tumekuja kuibadilisha”. Aliongeza Dcom

TanaPlay ni kampuni ya Muziki hapa nchini ambayo imefingua dtudio zake hivi karibu za kurekodi audio pamoja na video, Huku wakitegemea kuzindua kampeni maalumu ya Mapinduzi ya Muziki wa Injili Hivi karibuni.