Site icon A24TV News

TCRA YATOA TAHADHALI DHIDI YA MATAPELI WANAOJIFANYA NDUGU.

Na Doreen Aloyce, Dodoma

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA imetoa wito kwa jamii kuwa na kumbukumbu na watu ambao waliwasajilia laini za simu kwa kutumia kitambulisha cha Nida maana wanaofanya utapeli ni watu wao wa karibu ..

Hayo yameelezwa Jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Jabir Bakari alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA na maendeleo ya Mawasiliano.

“Niwasihi watanzania kuweni makini na matapeli kila siku watu wanalia kuibiwa wanapigiwa simu na watu wao wa karibu na matokoeo yake wanatapeliwa”alisema Bakari.

Aidha Mamlaka hiyo imesema kuwa Utoaji wa huduma za mawasiliano ni wa ushindani hivyo umesababisha kuongezeka kwa idadi ya mitandao, matumizi ya TEHAMA na aina za huduma zinazotolewa kwa Wananchi,
Taasisi na Serikali kwa ujumla.

“Kuenea kwa huduma hizi kunawezeshwa na uwepo wa Sera imara, sheria nzuri na mifumo wezeshi ya kiusimamizi na utoaji leseni,

TCRA imeendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia malengo yaliyoainishwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa (FYDP III) kwenye sekta ya mawasiliano, ambayo utekelezaji wake unahusisha mchango
wa TCRA kwenye uchumi ikiwa ni pamoja na Kuimarisha miundombinu ya mawasiliano na upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa lengo la kuboresha uchumi wa kidijiti na uchumi wa buluu

Pia Kuendelea kuweka mazingira bora ya ushindani kwenye sekta ya mawasiliano ili wananchi wengi waweze kumudu gharama za huduma za mawasiliano,”alisema.

Kugawa rasilimali za mawasiliano, ikiwa ni pamoja na masafa na kutoa leseni kwa watoa huduma zinazowezesha kuongeza idadi ya watumiaji wa intaneti ili kufikia
lengo la asilimia 80 ifikapo 2025.

Aidha amesema kuwa Ufuatiliaji na Utekelezaji Katika kipindi cha kuanzia Julai 2022 mpaka Juni 2023, TCRA imeendelea kuwasimamia watoa huduma za mawasiliano kwa kuhakikisha wanatoa huduma kwa mujibu wa masharti ya leseni zao pamoja na kuzingatia viwango vya ubora ambavyo vimewekwa kwenye kanuni na sheria zinazoongoza sekta ya mawasiliano nchini.

Aidha wamefanya maboresho makubwa ya mifumo ya udhibiti wa Sekta
ambapo kwa sasa tumejenga uwezo wa kufuatilia ubora wa huduma tukiwa ofisini,ili kuhahikisha watoa huduma za mawasiliano ya simu na intaneti, utangazaji (Radio na Televisheni) na posta wanatoa huduma kwa ufanisi na kwa kuzingatia ubora.

TCRA ilianzishwa chini ya Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Namba 12 ya mwaka 2003 baada ya kuunganishwa kwa iliyokuwa Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC)
na Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC).

Mwisho