Na Richard Mrusha
Mkurugenzi wa Shule za Alpha High School ,Fatina Mbwambo amesema Mwitikio ni mzuri wa watu kujitokeza kupima vipaji lakini utangazaji wake bado haujafanywa kikamilifu tofauti na nchi zingine wametangaza na watu wanagombania lakini hapa nchini ni mara ya kwanza..
amesema tangu kuingia mashine hiyo kwa mara ya kwanza nchini mwanzoni mwa Mwaka huu kupitia shule ya Sekondari Alpha tayari watu 31 wamepimwa vipaji.
Amesema waandishi wa habari kaweni mabalozi mkaitagazie umma kuwa Tanzania pia imapeta bahati ya kupata hiii teknolojia kwasababubu baadhi ya nchi wamewatumia waandishi wa habari kutangaza hii teknolojia.
“Kilichotuongoza kufanya hivyo mara nyingi tunaona watoto wanavipaji lakini hatujajua lakini watoto wa zamani ni tofauti na sasa wa zamani akiambiwa fanya hiki anafanya na wa sasa akiambiwa afanye hiki anaweza asifanye na Kama utampeleka anakotaka ataenda vizuri na baada ya kuona hayo mfano mtoto wa mtaani ukimwita na kumuuliza atasema anataka nini.
Amesema kuwa zamani wazazi walikuwa wanamuona mtoto wao anacheza anafikiri labda ni mchezaji wa mpira,akiimba anajua ni mwimbaji lakini sasa kimepatikana chombo ambacho kinatumika uhalisia wa kipaji cha mtu.
Mbwambo amesema mtoto akitumia kipaji vizuri kitampelekea na kumuongoza kwenye kile ambacho amejaliwa kama mzazi atamuongoza vizuri pia.
Kwa upande wake mtaalamu wa Kupima vipaji kwa kutumia mashine ya kupima vipaji inayoitwa Human Antropobiometric Machine, Profesa Humphrey Oborah amesema ili kupima kijapaji cha mtoto mashine hiyo inachukua picha na kuangalia ufanyaji kazi wa ubongo.
Amesema mtu anapopigwa picha inachukua muunganiko wa binadamu inachora ishara ya kufikirika na mwisho itaonesha ubongo wa mbele ambao umegawanywa sehemu mbili za kushoto na kulia.
Prof Oborah amefafanua kuwa Sehemu ya kushoto inawakilisha sayansi na upande wa kulia inawakilisha sanaa na upande wa nyuma wa kulia unawakilisha uimara wa kiafya ambapo wacheza mpira,wakimbiaji inawahusu na upande wa nyuma wa kushoto inaitwa ubongo wa kufanya maamuzi.
Amebainisha kuwa upande wa nyuma wa kushoto huo unafikiri,unapanga ,kuweka mpango ambao kisaikolojia vipaji vyote ziko sehemu hizo nne.
“Kwa mtu ninachotaka kujua kitu kikitendeka kwenye mguu ishara ikitoka inaenda upande wa kulia au kushoto mbele au kushoto juu au chini nyuma na nikijua ishara kwenye mwili wako inakimbia haraka sana upande wa kushoto juu halafu unaona mtoto wa miaka minne na mitano atakuwa mwanasayansi ,”ameeleza
Mwisho.
Mwishoooo………