Site icon A24TV News

WADAU WA MIFUGO,UVUVI NCHINI BaDO WANAKUMBANA NA CHANGAMOTO ZA MASOKO.

Na Doreen Aloyce, Dodoma

BAADHI ya wadau wa Mifugo na Uvuvi Tanzania wamesema bado wanakutana na changamoto za masoko ya mazao yao hasa kutoka nchi za nje kutokana na kukosa fursa mbalimbali za kimataifa hali inayowaweka mbali na wawekezaji katika sekta ya kifedha ambazo kama wakikutana nazo wanaweza kuongeza mitaji yao nakuongeza tija ya mazao yao.

Wadau hayo yaliyabainisha Jijini Dodoma kwenye maandalizi ya kushiriki mkutano wa Jukwaa la chakula Afrika 2023 ambao kwa mara ya pili unafanyikia nchini Tanzania ambapo wameiomba serikali kuwakutanisha na wafanyabiashara kutoka nje za nchi kwa kuwapa kipombele cha nafasi za maonyesho ya kimataifa.

“Tunachangamoto nyingi katika sekta ya uvuvi lakini tunaamini mkutano huu mkubwa kufanyika Tanzania ambao utahudhuriwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan na baadhi ya Marsi kutoka nchi 15 tunaamini utatufungulia milango ya kujuana kibiashara na tutaweze kutatuliwa changamoto zetu ili nasi tuweze kuzalisha kwa wingi na kwa tija”.

Nae Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi Tanzania Angelina Ngalula aliitaja Sekta ya Uvuvi na Mifugo ni muhimu katika kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi kwa kuzalisha kwa tija ili nchi ionekana kimataifa katika sekta mbalimbali ikiwemo hiyo ambayo inafanywa na watu wengi huku akiwataka washitiki wajue wanataka nini katika mkutano huo na kama bado wajibange kujua manufaa watakayotokana nayo katika mkutano huo mkubwa kimataifa kwakua kwa baadhi ya ,iaka haukufanyika kutokana na changamoto ya ugonjwa wa Uviko 19 lakini sasa utafanyika Jijini Dar es salaam Tanzania Septemba 23.

“Kuangalia namna gani wanaboresha mazingira ya uwekezaji ili kuvutioa wawekezaji kuona vitendo zaidi na sio maneno bila vitendo kwakua ni mkutano wakiushindani kuonyesha faida za uwekezaji Tanzania na pindi watakapopenda kuja kuwekeza nchini wajue kile watakachovuna kwakua hakuna mtu anapenda kuwekeza bila kunufaika na washiriki mjiande vizuri kuongeza ushindani kimataifa ili mumpe moyo Rais Dk.Samia ambaye mara kadhaa ameonekana akitafuta wawekezaji na sasa wameanza kuja hivyo wakute uhalisia wa kile kinachosemwa kwenye mikutano mbalimbali anayoshiriki.”. Alisema Ngaluma

kwa upande wake Mwakilishi Mkazi ,Mwakilishi wa Wadau wa Maendeleo na Muwakilishi wa Benki ya Dunia kwa pamoja waliipongeza Tanzania nakuahidi kuendelea kutoa ushirikino wa hali na mali katika kuifanya Tanzania inaongeza ushindani kibiashara kimataifa ili kuhakikisha malengo walioyaweka wanayafikia na kuondoa umaskini Tanzania kwa watu kufanya shughuli zakujiajiri wenyewe katika sekta mbalimbali zikiwemo Mifugo na Uvuvi.

 

Kwa upande wake muwakilishi wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Viwanda na Bisahara Dk.Joseph Mhagama aliwashauri wasimamizi wa sekta ya Kilimo na Uvuvi kuhakikisha wanawasaidia watu wenye nia yakufanya shughuli hiyo ambayo inalenga kuongeza ajira na vipato kwa makundi ya wanawake na vijana nakupunguza hali ya utegemezi kwenye jamii ambayo bado.

Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri wa Usalama wa Chakula linalomshauri Rais kuhusu Chakula ambaye pia ni Waziri Mkuu mstaafu Mhe.Mizengo Pinda alisema swala la usalama wa chakula si ajenda ya Tanzania pekee bali ni la Dunia nzima kwasababu lilianza kuchomoza 2021 kwa viongozi wakuu wa nchi kukutana na kukubaliana lifanyike kwa nchi zote wanachama wa jambo hilo.

“Sekta binafsi itoe kipaombele na itangulie ione inashiriki vipi kuhusu uboreshaji wa sekta ya uvuvi na mifugo na kuwaonyesha washiriki namna Tanzania onavyoshughulika na mazao hayo ambayo kwa baadhi ya nchi bado haijaonekana umuhimu wake na ndio maana serikali imewekeza zaidi kwa vijana na wanawake .

Kuwa uwekezaji huo ni kwakua ndio wazalishaji wakubwa wa mali hasa wanafanya vizuri katika sekta ya kilimo hivyo tushiriki pamoja kuisimamia huku akiishauri serikali iweke pia nguvu katika sekta ya Nyuki ambayo inazlisha asali zinazotumika katika kutengeneza vitu mbalimbali na wengine ufanya tiba ya magonjwa mbalimbali.” Alisem Mhe Pinda

“Nimefanikiwa kupita maeneo mbalimbali yanayijihusisha na mazao ya mifugo nimeona mabadiliko makubwa nakua mteja mzuri wa bidhaa hizo ambazo hazijapewa kipaombele sana lakini ndio zinazosaidia sana katika kuchagiza uchumi wa nchi hivyo ni vyema zisisahaulike an ziangaliwe vizuri ili kusaidi ajira kwa watanzania na sio kusubiria kuajiriwa pekee.” Alisema

Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega aliwataka wafanyabiashara wa sekta ya Uvuvi na Mifugo watakaoshiriki mkutano huo mkubwa kimataifa kuhakikisha wanaondoka na faida kutoka kwa washiriki wa nchi zingine ambao watakuja kujifunza shughuli hizo na kila mtu awe mwepesi wakuchangamkia fursa yeyote itakayoonekana ili kuweza kuongeza mitaji yao kwani watakutanishwa na wawekezaji katika sekta ya fedha.

“Wadau niwasihi msizubae mkakosa fursa mbalimbali zitakazoonekana siku ya mkutani ikli muongeze ujuzi kwa njia ya tehama na teknolojia mpya ambazo sisis bado hatujazifikia na itawasaidia na nyie kujulikana na kujipatia wateja kutoka mataifa mengine nje ya Tanzania ambalo ndio dhumuni kubwa la mkutano huo ambao Rais wa Tanzania alijitoa kimnasomaso kuomba ufanyike Tanzania awamu hii kwakua tuko tayari kuundaa hata kama tunakutana na changamoto tujitahidi kuzitatua na kusonga mbele zaidi ili kama nchi tufanikiwe.” Lisema Mhe.Ulega


“Alisema Mifugo ni Avuvu inazalisha fedha nyingi sana ambazo zinapotea kutokana na kutofahamu njia bora zakufanya biashara hiyo kwakua bado wanakutana na changamoto mbalimbali zikiwemo za uhaba wa mitaji, uhaba wa malisho, uchache wa malambo na tabia nchi hali ambayo imeisukuma serikali kuangaklia namna bora yakuboresha nakuweka mazingira wezeshi kwa kuongeza mikopo katika sekya hiyo kwani mpaka nsasa tayari watu Milioni 4.5 wamefanikiwa kuajiriwa au kujiajili kwenye mnyoror wa dhamani wa sekta ya mifugo na uvuvi..”alisema.

mwisho .