Site icon A24TV News

WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU WATAKIWA KUSOMA TAREEH ILI KUJUA HISTORIA YA DINI YAO.

Na Mwandishi wa A24Tv .TANGA –

Waumini wa dini ya Kiislamu kote  dunuani  wameaswa kujenga mazoea ya kusoma na kuchambua matukio ya tareekh ili kuweza kujua historia ya Dini yao ya vizazi  vyake.

 

Hayo yameelezwa leo Mkoani Tanga na Mudir wa Muasas Sheikh Shaffi Muhammed Nina wakati wa maandamano ya Maombolezi ya kumbukumbu ya kifo cha mjukuu wa Mtume Muhamad ( S.A.W ) Imam Hussein ( A.S) aliyefariki mwaka wa sitini na moja Hijiria.

 

Sheikh Shaffi amesema  kuna haja ya kusoma na kuchambua tareekh kwa kuwa vitabu vya mwenyezi Mungu vilikuja  vikiwa salama lakini kulingana na siasa za walimwengu wamekuwa wakibadili maneno ya vitabu hivyo ila  Qur-an ilisimamiwa vyema na Imam Hussein (A.S) na kubaki Quran kama ilivyoshushwa na Uislamu kubaki kuwa Uislamu.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki katika siku hii ya Ashura akiwemo kiongozi  wa taasisi ya Almustafa Khairiya  Sheikh Alli Amari Mwazoa na Shekhat Othmani kwa pamoja wamesema kupitia siku hii Waislamu wanapaswa kujifunza kuwa na umoja na kuacha udhalimu baina yao.

Mamia ya Waislamu katika mitaa na vitongoji mbalimbali wilaya ya Tanga Mjini wameshiriki shughuli ya siku ya Ashura ya kukumbuka siku ya kuuliwa shahidi mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW), Imam Hussein bin Ali bin Abi Twalib (AS), Imam Husain AS aliuawa shahidi kikatili na kinyama katika jangwa la Karbala nchini Iraq akiwa na umri wa miaka 57 baada ya kuongoza mapambano ya kishujaa ya ushindi wa damu mbele ya upanga.

mwisho