Site icon A24TV News

WAZIRI MKENDA SERIKALI INAJALI ULINZI NA USALAMA KWA WAYOTO WAKIKE NA KIUME

Na Geofrey Stephen ,Monduli

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Professa Aldof Mkenda amesema kuwa serikali inajali ulinzi na usalama wa mtoto wa kike sehemu ya kazi na ndio maana inasisitiza muhimu wa elimu kwa jinsi hiyo.

Waziri Mkenda ameyasema hayo Wilayani Monduli Mkoani Arusha katika  Chuo Cha Maendeleo-Mto wa Mbu{FDC} wakati akizindua mwongozo na Mafunzo ya Ulinzi na Usalama wa Mwanamke na Vijana katika kupiga vita unyanyasaji kijinsia na kingono.

Alisema serikali inajali na kutamnua  ulinzi na usalama wa mtoto wa kike na kiume katika mafunzo ya taasisi mbalimbali Nchini ya ufundi stadi na ndio maana inaingia gharama kubwa kutafuta wataalamu kutoka nje kuja kutoa elimu bora kwa jinsi hizo hapa nchini na kupata wakufunzi wengine kwenda nje kupata ujuzi zaidi kwa maslahi ya Nchi.

Waziri alisema na kusisitiza kwa wanafunzi waliohitimu katika Chuo hicho kuhakikisha wanajiajili ili wawe mabalozi wazuri kwa wenzao ili waweze kujiunga na vyuo mbalimbali hapa nchini vya ufundi stadi na kuwaeleza kuwa unyanyasaji wa kijinsia na kingono imebaki historia kwani serikali inapiga vita kwa nguvu zote

Alisema ni wajibu wa serikali kuhakikisha vyuo vyote Nchini vya ufundi stadi vinatoa elimu bora kwa vijana wa kike na kiume ili waweze kuajiriwa  na kujiajiri pindi wanapoimaliza elimu yao ili kupinguza wimbi la ukosefu wa ajili.

Mkenda alisema Wizara yake kwa kushirikiana na serikali ya Canada kupitia Jumuiya ya Vyuo na Taasisi za Ufundi Canada imeanda Mwongozo wa Ulinzi na Usalama kwa wanachuo  katika Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi,Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi na Vyuo Vya Ualimu.

Alisema Muongozo huo umeainisha mikakati ya utekelezaji na kutoa maelekezo kwa wadau ili kuweka kipaumbele katika ulinzi,usalama na ustawi wa wanachuo hivyo Wizara inatarajia kuwa vyuo husika,wadau na washiriki wa maendeleo watatumia mwongozo huo kuimarisha ulinzi na usalama ili kupunguza vitendo vya ukatili na unyanyasaji kwa jinsi hizo.

Naye Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya na Taasisi ya Vyuo Nchini Canada,Denise Amyot kwanza aliishukuru serikali ya Tanzania kwa kutoa ushirikiano mkubwa katika ulinzi na usalama wa mtoto wa kike na kusema kuwa serikali ya Canada itakuwa mstari wa mbele katika kutoa wataalamu katika vyuo mbalimba hapa Nchini ili kuiwapa elimu ya ufundi stadi.

Amyot alisema vyuo 12 hapa Nchini viko katika mpango wa kutoa elimu ya ufundi stadi kutoka kwa wataalamu wake kutoka nchini Canada lakini malengo ni kutaka vyuo vyote nchini kunufaika na Malengo hayo.

Rais alisema kuwa mradi huo wa miaka saba 2021-28 unatekelezwa na Jumuiya ya Vyuo na Taasisi za Ufundi Canada{CIC} kwa ushirikiano wa karibu na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Tanzania{MOEST} kupitia idara ya elimu ya ufundi na Mafunzo ya Ufundi stadi{DTVET} mradi huu unafadhiliwa na serikali ya Canada.

Amesema lengo kuu la mradi ni pamoja na Kuboresha Ushiriki wa Wanawake na Wasichana kwenye shughuli za Kiuchumi Nchini Tanzania na utaimarisha njia mbadala za elimu,ajira na kujiajili na Ujasiriamali kwa wanawake na wasiachana.

Naye Mdau wa elimu Wilayani Monduli,Stella Mollel alisema kuwa Ulinzi na Usalama kwa mtoto wa Kike katika vyuo na taasisi mbalimbali Nchini kunaweza kumsaidia kwa asilimia kubwa mtoto wa kike kujiamini hivyo ufadhili unaofanywa na serikali ya Canada na Tanzania unapaswa kupongezwa kwa asilimia kubwa hususani kwa jamii ya kifugaji.

Mwisho .