Na Mwandishi wa A24Tv
Dkt. Kijaji amesema hayo Julai 26,2023 alipotembelea Kiwanda cha Mbolea ITRACOM kilichopo Nala Jijini, Dodoma kujionea uzalishaji wa mbolea katika kiwanda hicho.
Aidha Amekipongeza Kiwanda hicho kwa utengenezaji wa mbolea usiokua na mchanganyiko wa asilimia 100 ya madini, bali asilimia 50 ni samadi na asilimia 50 ni madini ambao unaleta uhai wa ardhi kwa uasili na ubora wake.
Amesema baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Kiwanda hicho kwa awamu ya kwanza, kitaweza kuzalisha Tani millioni 1.2 kwa mwaka huku matumizi ya ndanj ya nchi ni Tani 650,000 hivyo hakuna sababu yakuagiza mbolea nje ya nchi.
Aidha Dkt. Kijaji amesema amezikaribisha nchi za Afrik Mashariki na Afrika kwa ujumla ikiwemo kenya ambayo tayari imeshanunua tani 3000 za mbolea kununua mbolea kutoka ITRACOM Mbolea ya Dodoma Tanzania.
Naye Mkurugenzi wa ITRACOM Bw Nduwimana Nazaire ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kutambua juhudi za uzalishaji wa mbolea katika kiwanda hicho na ameiomba Wizara ya Viwanda na Baishara kushirikiana na Wizara zingine katika juhudi za usambazaji wa mbolea hiyo.
Mwisho