Site icon A24TV News

BREAK NEWS !ASKOFU MKUU MPYA WA KKKT NI MALASUSA AWABURUZA WENZAKE KWA KURA NYINGI ZAIDI 167

Na mwandishi wa A24Tv Arusha.

Jopo la wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 21 wa kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) umemchagua kwa kishindo  askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dr Alex Malasusa kuwa mkuu mteule mpya wa KKKT kupokea nafasi ya Askofu Dkt Frederick Shoo aliyestaafu baada ya kumaliza muda wake wa uongozi  wa kanisa la Kkkt .

Mwenyekiti wa uchaguzi huo iliyofanyika Arusha Askofu Amon Mwenda alisema Askofu Malasusa ameshinda Kwa kura 167 sawa na asilimia 69.3 ya kura zote 241 zilizopigwa huku askofu Abednego kesho Mshahara akipata kura 73 sawa na asilimia 30.3.


Askofu Malasusa anarejea kwenye nafasi hiyo tena ,nafasi ambayo alikwisha tumikia kwa uwongozi  kati ya mwaka 2007 hadi 2015 alipomaliza muda wake na kumkabidhi Dkt Shoo.

Mwisho .