Site icon A24TV News

BILIONI 37 KUTOKA KWA RAIS SAMIA ZAFUFUA MRADI WA KUFUA UMEME KIKULETWA WILAYANI HAI

Na Geofrey Stephen Hai .

Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi cha bilion 37 kwa ajili ya kufufua Ujenzi wa Kituo cha kuzalisha Umeme kilichoanzishwa mwaka 1930
cha Kikuletwa pamoja na  chuo cha Ufundi wa umeme na mitambo kitakachochukuwa zaidi ya wanafunzi 600 ambacho kinaenda kuzalisha
wataalamu watakaotekeleza Miradi ya kimkakati ikiwemo bwawa la Mwalim Nyerere JNHPP.

Hayo yameelezwa  na Mkuu wa Wilaya ya Hai Amiri Mkalipa alipotembelea miradi unaotekelezwa na Chuo cha Ufundi Arusha ATC ambao utazalisha megawati 1.65 katika kijiji cha Chemka Kikuletwa
wilayani hai mkoani Kilimanjaro .

Amesema Mradi huo utakapokamilika utasaidia chuo kuuza umeme na wananchi wanaozunguka kunufaika na huduma hiyo jambo ambalo kituo
hicho kitazalisha wataalamu ambao watasaidia katika miradi mbalimbali itakayotekelezwa na serikali hapa nchini.

“Katika utekelezaji wa mradi huu lazima muhakikishe uzalendo unawekwa mbele sanjari na matumizi sahihi ya fedha bila kusahau kumaliza ujenzi ndani ya muda uliopangwa  ili manufaa ya Kituo hichi yaweze kuwanufaisha kizazi kijacho tofauti na awali ulipotekelezwa”

Mkuu wa chuo cha Ufundi Arusha ATC
Dkt.Mussa Chacha  amesema  mradi huo wa kituo cha umahiri kuzalisha Wataalamu wa nishati jadidifu watakaokuwa na uwezo wa kufanyakazi na kuzisaidia nchi za jumuiya ya Afrika mashariki na
duniani kote kwenye miradi mikubwa ya umeme ya kimkakati.

Amesema kwamba mradi huo unatarajiwa kumalizika mwezi wa Oktoba mwaka 2023  huku akimtaka mkandarasi kuendeleza kazi kwa kasi ili kuweza kumaliza ndani ya muda uliopangwa sanjari na kuhakikisha wanailipa halmashauri mapato yake.

“Tumejipanga kuhakikisha ujenzi unakamilika ndani ya muda uliopangwa sanjari na maagizo ya Mh.Mkuu wa wilaya ya hai yanatekelezwa kwa
haraka ili kuondoa changamoto za mapato ya halmashauri ambayo mkandarasi hajalipa tokea kuanza ujenzi wa chuo”

Mkandari anayetekeleza mradi huo Enginia Sumbuka Joseph amesema licha ya mradi kuchelewa kuanza kutokana na mwamba wanzo wa mradi wataakikisha mradi huo utakamilika kwa muda ulio pangwa

Amesema serikali iyendelee kuwa na imani kwao kwani kufikia October 25 Mwaka 2023 mradi utakua umekamilika na kukabidhiwa rasmi kwa chuo cha ufundi Arusha Atc .

Kwa Upande wake Mjukuu wa Mmoja ya waanzilishi wa Kituo hicho  cha kuzalisha Umeme Kikuletwa aliyefika kutembelea ambacho kilijengwa mwaka 1930 na wajerumani WOLF LEACK kutoka ujerumani amesema kwamba Babu yake alikuwa mkandarasi alietekeleza mradi huo wa kituo cha
kuzalisha umeme ambapo baba yake alizaliwa hapa nchini mkoani Kilimanjaro wilaya ya Moshi mwaka 1936 wakati wa Ujenzi wa kituo

Mwisho