Na Richard Mrusha Mbeya
MKUU wa Wilaya ya Ludewa Victoria amesema kubwa Wilaya ya Ludewa nao wanashiriki maonyesho haya ya Kimataifa ya kilimo Nane nane ambayo yanafanyika hapa Jijini Mbeya na kesho ndiyo kilele cha maadhimisho haya ambayo yatafungwa rasmi na Rais Samia wa Jamhuri ya muungano Samia Suluhu Hassan.
Amesema kuwa kama mkuu wa Wilaya ya Luwa leo agost 7,2023 amepata wasaa wa kutembelea mabanda mbalimbali likiwemo banda la tigo ,na kuongeza kuwa tigo ni wadau muhimu katika kufikisha na kurahisisha mawasiliano kwa wananchi.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema kubwa pia naye amepata elimu juu ya product mpya ya tigo kuhusiana na masuala ya kilimo.
“Ombi langu ni kuomba tuzidi kufahamu namna ambavyo wakulima kupitia vyama vyao vya ushirika AMCOS vyama vya Ushirika wanaweza kunufaika na huduma zinazotoewa na tigo kwa maana ya mikopo hasa kwenye uwezeshwaji wa pembejeo ili wakulima waongeze tija kwenye kilimo.
Ametumia fursa hiyo kuwataka kuwataka tigo na wananchi kwa ujumla waendelee kujifunza na kutoa huduma hasa za kilimo kwa wakulima kwa maslahi mapana ya wakulima wenyewe na Taifa kwa ujumla,kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa,kuleta ajira.
Aidha ameishukuru kampuni hiyo kwa kupeleka mawasiliano katika eneo la Lupingu wilayani humo ambalo halikuwa na mawasiliano kabisa.
Hata hivyo ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha Tigo kwenye wilaya yake kuendelea kuboresha za mawasiliano.
Mwisho.