Site icon A24TV News

DON RESOURCES TANZANIA COMPANY LTD YAWATAKA WAKAZI KUCHANGAMKIA FURSA YA MADINI.

Na Richard Mrusha, Ruangwa

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Donresources Mukhusin kikulu amesema uwepo wa maonesho ya madini na uwekezaji mkoa wa lindi umefungua fursa kwa wakazi wa mkoa wa lindi na ukanda wa kusini kwa ujumla wake kwenye sekta ya madini.

Amesema wao kama kampuni ya kizawa wameata fursa ya kushiriki kataki maonesho hayo kazi kubwa yanayoifanya wamewekeza kwenye sekta ya madini haswa kwenye usambazaji wa vifaa na kufanya tafiti mbalimbali kwenye maeneo ya madini na ushauri.

Amesema maonesho hayo yameweza kufungua fursa na kuelekea kutambua na kugundua maeneo muhimu ambayo yanaonyesha yana madini ili shuguli za uzalishaji ziweze kufanyika katika maeneo hayo ambayo yamefanywa tafiti.

Ndugu wanahabari leo hii tupo ruangwa kwa kipekee tunawashukuru waandaaji wa maonesho haya tumeweza kukutana na taasisi ya uwezeshaji kiuchumi ambayo imenzishwa hapa ruangwa

Amesema kazi yake ni kuweza kutambua na kutafuta kampuni au wadau mbalimbali wa kitanzania ambao wanapenda kuwahusisha kwa kuwapatia kile ambacho kinastahili ili waweze kuwangunisha kwa lengo la kufanya kazi kwa pamoja kwa kupita umoja huo itakuwa rahisi kutambulika na kupata ushirikiano mkubwa na kuweza kuyaonyesha yale wanayoyafanya

Ameongeza kuwa hivyo kutoka sasa na kwenda mbele watakuwa na mchango mkubwa katika ukanda wa kusini lakini pia watakuwa na mchango mkubwa zaidi kwa nchi yao ya Tanzania kwasababubu watakuwa wamefahamika zaidi.

Kwa upande wake Meneja Rasimali watu na utawala kutoka kampuni ya Akmenite ambayo inajihusisha na ununuzi wa madini na kuchakata madini
Coletha Mwita amesema lengo lakutembelea Maonesho hayo ya madini kwa lengo lakujitangaza na kutafuta watu ambao watawauzia hayo madini na sisi tutayanunua kwa bei elekezi iliyopangwa na Serikali.

“Tupo hapa kuangalia watu ambao wapo tayari kufanya kazi na sisi ambapo pia tunawasaidia wachimbaji wadogo ambao wanaweza kuchimba wameanza kuchimba lakini hawezi kumaliza ile shughuli pale alipofikia kama atahitaji msaada kwetu tutamsaidia ili aweze kumaliza ile kazi lakini pia tutanunua mzigo wake kwa bei nzuri sana hivyo basi tunawakaribisha wachimbaji wadogo wote waje watuuzie madini yao,”amesema Coletha

Mwisho