Na Richard Mrusha mbeya
JESHI la kujenga Taifa (JKT) na wizara ya kilimo wametiliana saini mkataba wa mashirikiano katika kutekeleza mradi wa mashamba makubwa kuwezesha vijana kilimo biashara-Building a Better tomorrow (BBT) mbele ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na amiri jeshi mkuu Mh.Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa (JKT) Meja jenerali Rajab Mabele amesema jeshi hilo limeanza kutekeleza agizo la amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Dk.Samia Suluhu Hassan na kuhakikisha vijana wanaotoka makambini wanajengewa uzalendo wa kitaifa na kunufaika na fursa zilizopo katika sekta ya kilimo,Mifugo na Uvuvi kupitia mradi huo wa BBT unaotekelezwa na wizara ya kilimo.
Meja jeneral Rajab Mabele amesema hayo kwenye kilele cha maonesho ya kimataifa ya kilimo nane nane 2023 jijini Mbeya baada ya hotuba ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu hassan ambapo amesema kuwa Wizara ya mifugo na uvuvi ni kuhakikisha kwamba hizi wizara mbili zinaungana pamoja ili kuweza kuhakikisha kuwa vijana wa kitanzania wanaoandaliwa katika utaratibu wa (BBT) kwa upande wa kilimo BBT na kwa upande wa Mifugo na Uvuvi.
”Tunahakikisha kwamba kwanza wanapata uzalendo katika Jeshi la kujenga Taifa, wapate ukakamavu ili wanapokwenda katika kazi zile ambazo zitakuwa za shamba waweze kuwa na uvumilivu wa kufanya kazi zile,” alisema Meja jenerali Rajab Mabele Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa (JKT).
Hata hivyo, mkuu wa huduma za sheria kutoka jeshi la kujenga Taifa (JKT) kanali Projest Rutaihwa alisema kuwa kupitia maonesho hayo wameweza kusaini makubaliano na wizara ya kilimo pamoja na wizara ya mifugo na uvuvi na kuongeza kuwa mashirikiano hayo ni katika taratibu za BBT ambazo zimezinduliwa hivi karibuni na serikali na kwamba Jeshi la kujenga Taifa katika makubaliano na wizara hizo wanakuwa wanachukua vijana wanawafundisha mambo ya uzalendo,ukakamavu na stadi za kazi.
Aidha Rutaihwa alisema kuwa kwa pamoja watakauwa na majukumu ya pamoja ambapo watakuwa wanaratibu uendeshaji wa mafunzo hayo na kwamba wanategemea kuwa mashirikianao hayo yatafikia pazuri.
Kwa upande wake Naibu wakili mkuu wa serikali Sarah Mwaipopo alisema serikali itaendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali katika utatuzi wa migogoro mbalimbali ikiwemo migogoro ya ardh.
” Sisi tupo hapa kwa sababu tunasimamia masuala ya utatuzi wa migogoro, na moja ya migogoro ambayo tunaisimamia au ambayo inajitokeza mara kwa mara ni migogoro ya ardhi kwa mana hiyo ofisi yetu ipo ili kuhakikisha kwamba tunatatua migogoro yote ambayo inafunguliwa na serikali,” alisema Sarah Mwaipopo Naibu wakili mkuu wa serikali.
Mwisho.