Alisema ujio wa madaktari hao ni fursa kwa hospital ya Seliani na serikali pia ni faraja kwa wagonjwa wa Mifupa na Nyonga kwa Nchini kwa ujumla na kusema kuwa amewashukuru wale wote waliofanikisha hilo kwani watakuwa wamewaokoa wagonjwa wengi waliokuwa na magonjwa ya mifupa,magoti na nyonga kuepusha gharama kubwa za matibabu zinazofikia takribani Milion 60 hadi 80.
Alisema mbali ya kufanya upasuaji pia watakuwa wakifanya somo darasa kwa madaktari wa Hospital ya Seliani ili kupata uelewa zaidi ya upasuaji wa magoti na nyonga na hiyo ni fursa kwa madaktari wa kitanzania waliopo katika hospitali hiyo iliyopo Jijini Arusha.
Mwisho.