Site icon A24TV News

MSAMAHA WA KODI USAJILI WA MIRADI TIC

Na Richard Mrusha. Ruangwa

WAWEKEZAJI nchini wameshauriwa kusajiri miradi yao kupitia kituo cha uwekezaji TIC ili waweze kupata msamaha wa kodi inayotolewa na Serikali kupitia TIC.

Akizungumza leo 24 Aug 2023 katika maonyesho ya madini yanayofanyika katika viwanja vya soko jipya kilimahewa wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

Afisa muwekezaji mkuu TIC Kanda ya Mashariki Griyson Mtimba amesema kuwa wapo katika maonyesho ya madini na uwekezaji yanayofanyika katika Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi kwa ajili kufutia na kuhamasisha wawekezaji wa ndani na wa nje waweze kuwekeza Tanzania lakini pia katika mkoa wa Lindi.

Amesema pia hao kama TIC wana jukumu wanafanikisha uwekezaji kwakutoa vibali mbalimbali kwakushirikiana wenzao wa taasisi mbalimbali za Serikali ikiwemo Nida uhamiaji,osha na Taasisi nyingine ambazo zipo kituo cha mahala pamoja cha kutoa huduma zakufanikisha uwekezaji.

Aidha amesema kuwa kupitia maonyesho hayo muitiko umekuwa mkubwa hasa kwa wawekezaji wa ndani ambapo wamewapa elimu ya uwekezaji na namna nawaweza kusajiri miradi TIC.

“Tunawahamasisha wawekezaji wa ndani waje wasajiri miradi yao TIC huku kuna punguzo la kodi hasa wanapoaagiza vifaa vyao kutoka nje ya nchi nasi kama TIC tupo tayari kushirikiana nao hasa wakishapata cheti cha uwekezaji kutoka TIC ikiwemo vifaa vyakuchakata madini na miradi mbalimbali”amesema Mtimba

Kwa upande wake Afisa mwandamizi muhamasishaji wa uwekezaji wa ndani Latifa Kigoda amesema wapo kwenye maonyesho hayo kwa lengo la kuwapa habari njema kutoka kwa mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kwamba ameboresha mazingira ya uwekezaji ikiwa ni pamoja na kupunguza mahitaji ya yakuweza kujisajiri na TIC.

Latifa ameongeza hapo awali ilikuwa ili mwekezaji akithi mtaji wakuweza na kujisajiri TIC lazima thamani ya mradi wake uwe milioni miambili ila baada yakuonekana muamko wa wazawa mdogo mh Rais amepunguza kutoka milioni mia mbili na kufikia milion mia moja.

“Pia ninaomba niwafahamishe wana Lindi kituo cha Uwekezaji wa Tanzania siyo Taasisi ya wageni peke yao kama walivyo wengi walivyokuwa na hiyo dhana TIC ni kwa ajili ya wawekeza wazawa ambao ni watanzania wenyewe pamoja na wawekezaji wakutoka nje ya nchi “amesema latifa

Mwisho .