Na Ahmed Mahmoud
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amekabidhi tuzo mbili Kwa Shirika la bima la Taifa ikiwa ni kutambua mchango wao Kwa ufanisi mkubwa wa kifedha na kiuendeshaji pia mabadiliko makubwa ya kiutendaji kuongeza ufanisi tija na ubora wa huduma katika kipindi kifupi.
Hayo yameelezwa Mara baada ya kupokea tuzo hiyo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Bima nchini Dkt.Elirehema Dorie wakati wa Kikao Kazi cha wenyeviti wa Bodi na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma nchini kinachoendelea Kwa siku tatu Jijini Arusha.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji huyo tuzo zinaakisi Kazi zinazofanywa na Shirika letu la bima ni Kazi kubwa lakini ni Kazi ambayo imelenga kuongeza tija Faida ufanisi na ubora wa huduma tunazotoa
Hata hivyo alibainisha kwamba kampuni hiyo Imekuwa ikimthamini mteja na kumuweka katikati ya shughuli zake Kwa kuhakikisha inampa huduma Bora na hii ni chachu Kwa vile tunavyovifanya na Kwa Sababu tumepewa hizi tuzo na Rais maanake ni kwamba Kuna Kazi kubwa ya kufanya mbeleni.
“Kuhakikisha wateja wetu wanafurahia huduma zetu sanjari na wateja wetu wanaendelea kupata huduma zetu zenye ubunifu,ubora za uhakika lakini huduma zenye kujali muda Kwa Sababu huduma ya bima inathamini Sana kujali suala la muda katika ulipaji wa Madai, uandikishaji lakini katika utoaji wa elimu”
Alifafanua la pili ni kuzidi kuboresha muonekano wa Shirika la Bima la Taifa na kuzidi kuboresha mapato na Faida Kwa hiyo ukuaji wa biashara na ukuaji wa kampuni sanjari na kuwaendeleza wafanyakazi Ili waendane na Kasi na ukuaji wa kampuni.
Alisema Shirika hilo linanafsi kubwa ya utoaji elimu Kwa jamii na hilo ombwe ambalo linaonekana linatokana na NIC kipindi cha nyuma ambacho haikufanya vizuri Kwa hiyo makampuni mengi ambayo yaliingia nchini kufanya biashara yalithamini zaidi kupata Faida nakutokuwapa elimu ya kutosha Watanzania.
Alisema Sasa NIC ipo vizuri na wamekuwa wakitoa elimu Kwa Watanzania Kwa Sababu tunahitaji jamii inayoelewa umuhimu wa huduma za bima Kwa manufaa yao na manufaa ya Taifa wakitambua hii ni nchi yetu na Shirika la Watanzania inayomilikiwa na Serikali yao hivyo kila mtanzania ana umiliki wa Shirika.
“Kwa hiyo sote tunawajibu sawa wa kumkinga kwanza kumpa elimu sahihi Kwa kuchagua bima sahihi Kwa Maendeleo yake ndio maana tuna bidhaa mpya ya bima ya kilimo na nyinginezo”. alifafanua