Site icon A24TV News

TTCL YAJIDHATITI MABADILIKO YA KIDIJITI KWA KUANZA KUTOA HUDUMA ZA INTERNET MAJUMBANI NA MAENEO YA WAZI

Na Ahmed Mahmoud
SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeanza kujidhatiti kupamba na mabadiliko ya kiuchumi ya Teknolojia ya Tehama  duniani kwa kuanza kutoa huduma ya intaneti majumbani na maeneo ya wazi.
Mkurugenzi wa Biashara Shirika la Mawasiliano nchini TTCL ,Vedastus Mwita amesema hayo leo jijini Arusha alipohudhuria kikao Kazi cha wenyeviti wa Bodi na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma,na Binafsi.
Mwita alisema kuwa TTCL imejipanga kuhakikisha intaneti inapatikana majumbani na maeneo ya wazi ili kumwezesha mwananchi kupata mawasiliano popote alipo na hilo limewezekana kwa shirika hilo kuweka huduma hiyo katika Mlima Kilimanjaro na intaneti kuwa na kasi kubwa.
Alisema shirika hilo limeweza kuweka huduma hiyo katika kilele cha Mlima Kilimanjaro na kufanya watalii wengi wanaopanda mlima huo kufurahia huduma ya intaneti kileleni.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa baada ya kufanikiwa kwa asilimia kubwa kuweka Mkongo wa Taifa katika Mlima Kilimanjaro na kupata huduma ya intaneti katika mlima huo sasa TTCL imekuja na huduma nyingine ya kuweka huduma hiyo katika makazi ya watu yaani majumbani na maeneo ya wazi kama vile nyumbani ,sokoni ,stendi ,maeneo ya starehe na bei zimezingatia kipato cha mtanzania wa hali ya chini.
Alisema na kusisitiza TTCL inaunga mkono mabadiliko yatakayokuja kwani yatakuwa na jita kwa taifa na wao walishabadilika muda mrefu hivyo ujio wa mabadiliko hayo kwao sio kitu kipya bali ni kuongeza ufanisi zaidi kwani shirika hilo lilipewa cheti cha kuaminika kwa kutunza data duniani.
Mkurugenzi Mwita alisema wamekuwa wakifanya vizuri katika kutunza data na kusafirisha hivyo mipango iliyopo ya TTCL ya kutoa huduma ya Internet nyumbani na maeneo ya wazi yatakuwa ya viwango vya hali ya juu kwani shirika hilo limejipanga kikamilifu.
Tuna uthubutu wa kufanya vizuri katika kufunga Internet majumbani na maeneo ya wazi kwani Mkongo wa Taifa uliofungwa una uwezo mkubwa wa mawasiliano’’
‘’Niwatoe wasiwasi wananchi juu ya hilo kwani TTCL imejipanga kikamilifu kutoa huduma ya Interner mahali popote na kwa wakati wowote bila kujali hali ya hewa’’alisema Mwita.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) ,Professa Frederick  Kahimba alisema kuwa iwapo TTCL wanafanikiwa katika kuweka intaneti majumbani na maeneo ya wazi na mawasiliano hayo yakawa na nguvu nzuri huenda shirika hilo likaweza kuongeza imani kwa watanzania tofauti na awali.
Mwisho .