Site icon A24TV News

WAGONJWA 35 WAPATIWA MATIBABU BURE NYONGA NA MAGOTI MPANGO WA MAMA SAMIA LOVE

Na Geofrey Stephen Arusha
Wagonjwa wapatao 35 kati ya 200 waliojiandikisha , wamefanyiwa upasuaji wa Nyonga na magoti bure katika hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre ALMC, kupitia mpango wa mama Samia Love unaotekelezwa  na madaktari bingwa kutoka Marekani kwa kushirikiana na madaktari wa ndani.
Akiongea na vyombo vya Habari Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospital ya Arusha Lutheran Medical Center ALMC Godwel Kivuyo alisema kuwa wimbi la uhitaji wa huduma ya upasuaji kwa wagonjwa bado ni kubwa na katika awamu hii ya kwanza watafanya upasuaji kwa wagonjwa 50 na kati yao 35 tayari wameshafanyiwa upasuaji tangia kuanza kwa zoezi hilo Agosti 11 mwaka huu.
Alisema upasuaji umefanyika kwa mafanikio makubwa na wagonjwa wanaendelea vizuri na kila mgonjwa anayefanyiwa upasuaji kuna kuwa na madaktari wa ndani na changamoto kubwa kwa sasa ni muda kuwa mdogo na mahitaji ni makubwa.
Alisema madaktari wa kitanzania wakitoa msaada kwenye huduma za Dawa za usingizi wauguzi na madaktari hao kupata uzoefu na mafunzo Kwa kubadilishana uzoefu wa Teknolojia mpya Kwa pande zote.
Kwa Upande Wake Dkt.bingwa  Dkt.Steven Meyer Kutoka Taasisi ya mifupa STEMM nchini Marekani, aliendelea kumpongeza rais Samia  kutokana na moyo  wake wa kizalendo na huruma, kuruhusu matibabu ya kibingwa  kwa watanzania wenye kipati kidogo.
“Tunafanya upasuaji usiku na mchana kuhakikisha tunafikia malengo tuliojiwekea ya wagonjwa 50,tunafanya Kazi bega Kwa bega na wauguzi na madaktari wa kitanzania tukibadilishana uzoefu”
Naye Mratibu wa zoezi hilo la Upendo wa Rais Samia Suluhu,Lazaro Nyalandu alisema mpango wa mama Samia Love unalengo la kuwagusa wananchi mbalimbali hapa nchini baada ya huduma kuwa na mafanikio makubwa katika hospitali hii ya ALMC. 
Alisema mpango ujao wa siku za usoni wanatarajia kupokea madaktari bingwa wanawake ambao wameonyesha kuja kumuunga mkono Rais Mwanamke Afrika.
” Madaktari haqa bingwa wa magoti na Nyonga wamefurahia mapokezi na ukarimu wa Watanzania na wamewavutiwa kuja tena nchini na dhamira yao ni kwenda maeneo yote ya nchi Kutoa huduma za matibabu” .
Alisema madaktari  hao kutoka shirika la Operation Walk  limepanga kufanya makubaliano maalumu na wizara ya afya  Kwa ajili ya kuongeza wingi wa Timu zinazokuja kufanya huduma za matibabu na upasuaji Kwa Kanda mbalimbali hapa nchini.
Alisema kwamba wataendelea na dhamira hiyo Kwa madaktari wa hapa nchini na nje kufanya kliniki Kwa pamoja kwenye kila pembe ya nchi kuhakikisha Watanzania wanapata huduma Bora za matibabu ya kibingwa hususani ya Nyonga na magoti sanjari na magonjwa mengine.
“Mpango huo wa Mama  Samia Love una lengo la kuwagusa wananchi sio tu Kwa ukanda huu wa kaskazini  bali na kanda zingine nchini Kwa kuona ni jinsi gani madaktari wa Ndani na nje wanaweza kushirikiana “
Mpango wetu na Rais ni kufanya huduma hii iwe  endelevu kupitia kambi hizi ikiwemo hii ya Arusha kwa kutumia madaktari wa ndani kuwaimarisha .
Alishauri uwepo uwezekano wa kutumia madaktari bingwa wa ndani kutoka hospitali ya muhimbili ili kusaidia wagonjwa wasio na uwezo waliopo maeneo mengine  hapa nchini ambao wameshindwa kupata huduma za kibingwa.
Nyalandu alimpongeza rais Samia kwa kuondoa kodi ya takribani bilioni 2 kwa vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya sh,bilioni 12 vilivyoingizwa nchini kupitia madaktari hao bingwa ambapo wakimaliza muda wao wa matibabu vitabaki na kutumika hapa nchini
Ends…