Site icon A24TV News

WATANZANIA ANZISHENI MIRADI KWENYE SEKTA YA MADINI TIC

Na Richard Mrusha.Ruangwa

KITUO cha uwekezaji Tanzania (TIC) kimewataka watanzania kote nchini kuweza kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo kwenye sekta ya madini na kuweza kuzalisha ajira nakuongeza thamani Kwa lengo la kuanyanyua uchumi wa maendeleo nchini.

Akizungumza katika kongamano la uwekezaji lililofanyika katika viwanja vya soko jipya _kilimahewa wilayani ruangwa katika Mkoa wa Lindi ambapo yanafanyika Maonesho ya madini Afisa uwekezaji mkuu wa TIC Girson Ntimba Amesema ipo haja Kwa watanzania kujitokeza na kuwekeza katika sekta hiyo.

Afisa uwekezaji mkuu kutoka Kituo cha uwekezaji Tanzania TIC Girson Ntimba akizungumza katika kongamano la madini la uwekezaji katika maonyesho ya madini yanayofanyika wilayani Ruangwa.

Amesema kuwa kufanya hivyo kutaweza kuimarisha uchumi wa nchi na katika hilo tayari Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imelifanyia kazi kupitia kituo hicho cha uwekezaji na wanahamasisha watu wawekeze miradi ya nyenye thamani.

“Hapa niseme tu miradi yenye thamani ni kama kuzalisha vito,Pete hereni na vitu mbalimbali ambavyo vinaweza kutumika na tukapeleka nje Kwa ajili ya kupata fedha za nje “Amesema Ntimba

Nakuongeza kuwa “mh mgeni rasmi Waziri Dotto Biteko niseme kwamba sisi kituo cha uwekezaji katika kuhamasisha wawekezaji wa ndani ,katika maonyesho haya tumeweza kupata wawekezaji wawili ambao ni Jitegemee ambaye ameweza kusajili mradi na hatua zingine zinaendelea ili kuweza kupata kibali lakini Kuna Kampuni nyingine inaitwa Elianje ambayo nayo ipo kwenye mchakato wa kusajili ili kuweza kupata cheti cha uwekezaji “amesisitiza Ntimba Afisa uchumi mkuu

Amefafanua kuwa unapopata cheti cha uwekezaji unapata msamaha wa Kodi na lengo kuweza kutoa ajira kwahiyo Serikali inasamehe Kodi Kwa Sasa hivi ili mwekezaji aweze kuweka mradi na kuzalisha ,kuajiri watu na kuongeza kipato Chao na mwekezaji apate faida na Serikali ipate faida ,na kuweza kupata mapato ili badae aweze kulipa Kodi .

“Hivyo kusamehe Kodi nikuleta na kuwezesha miradi kuajiri watu wengi ili watanzania wanufaike na miradi hiyo Kwa misingi hiyo kituo cha uwekezaji kitatoa cheti ambacho kitafanya upate msamaha wa Kodi wakati wa kuingiza vifaa bandarini Kwa ajili ya mradi wowote ,iwe utalii au mradi wowote ambao unaongeza thamani na kuhakikisha unapata faida.

Ameongeza Kwa kuwataka wananchi ,wawekezaji kufika kwenye ofisi za kituo cha uwekezaji TIC ili kuweza kusajili miradi na mheshimiwa mkuu wa Wilaya aliweza kuhamasisha wadau kusajili TIC hivyo anawaomba watanzania kujitahidi kusajili miradi yao kituoni hapo.

Amesema kuwa Kuna manufaa makubwa Sana Serikali inaweza kusamehe Kodi ili kukufanya kuzalisha na kutoa ajira Kwa watu watanzania wanavyuo wanaomaliza waweze kupata ajira hivyo Waziri amesisitiza sana hilo kikubwa wajitokeze kwenye kituo cha uwekezaji kusajili ili kupata misamaha ya Kodi.

Mwisho.