Na Geofrey Stephen Arusha
CHUO cha Uhasibu Arusha (I.A.A),kimeeleza mafanikio makubwa ya elimu yaliyotokana na ongezeko la mitaala na kufanya pato la ndani kufikia sh,bilioni 26 sawa na ongezeko la sh,bilioni 15 kutoka mwaka wa fedha wa 2021/22.
Mkuu wa chuo hicho Profesa Eliamani Sedoyeka,amebainisha hayo wakati alipokuwa akizindua ripoti ya Chuo hicho na kuyataja mafanikio hayo kuwa ni pamoja na kujengwa Kituo kikubwa cha kisasa cha Habari na mawasiliano kwa nchi za afrika (ICT)ambacho kitaanza kufanyakazi mwakani .
Alisema mafanikio hayo yametokana na ongezeko la wanafunzi kukua na kufikia 13,000 na lengo ni kufikisha wanachuo wapatao 16,000.
Mafanikio mengine ni ,kujengwa kwa matawi ya chuo hicho (Campus) Dodoma,Babati,Songea,kuendelea na Ujenzi wa tawi la Ruvuma,kusomesha Wahadhiri,na watumishi wa kada mbalimbali.
Alisema ongezeko la Wanachuo,kutoa mafunzo ya Uhasibu na mafunzo ya mbinu za kisasa za Ulinzi wa nchi kupitia mtandao ,(Cyber security,) kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi yatakayotolewa kupitia chuo cha Polisi Moshi.
Alisema kuwa chuo hicho Katika mafanikio hayo kinasomesha Wahadhiri ngazi ya Uzamivu (PHD,52),masta,(9) digree ya kwanza (4) na watumishi wa kada zingine ili wafikie kiwango Cha digree,lengo ni watumishi wote wafikie madaraka ya juu ya Elimu,kuimarisha mkakati wa kusimamia na kuendeleza vyanzo vya mapato hayatokani na ada za Wanachuo lengo ni kuboresha mapato ya chuo.
Prof. Sedoyeka,alisema kuwa chuo kinatoa mafunzo ya Ulinzi wa nchi Kwa kutumia mtandao Kwa Jeshi la Polisi ili kuwawezesha kudhibiti vitendo vyote vya uhalifu ambapo masomo hayo yanatolewa Kwa Maafisa wa polisi wenye digree kupitia chuo cha Polisi Moshi.(CCP).
Alisema chuo kinaendeleza mahusiano na Jeshi la wananchi JWTZ,Jeshi la Polisi na lengo ni kuwezesha Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama kupata mafunzo mbalimbali chuoni hapo
Alisema kuwa mpango mkakati wa kuboresha chuo umewezesha chuo hicho kukusanya shilingi bilioni 26,ambayo inatokana na ongezeko la shilingi bilioni 15 la mwaka 2021/22 na hiyo inatokana na ongezeko la Wanachuo ambapo Kwa sasa chuo hicho kina Jumla ya Wanachuo 13,716
mafanikio mengine ni kuboresha mitaala ya masomo chuoni hapo ili iendane na wakati na tayari mitaala 30,ipo kwenye maboresho ambayo hufanyika Kila baada ya miaka mitano .
Ujenzi wa majengo ya matawi ya chuo hicho( Campus) yanatekelezwa Kwa fedha za ndani kupitia force account na pia benki ya Dunia imetoa mkopo wa Dola milioni 21fedha ambazo zinawezesha chuo na matawi yake kuboresha miundo mbinu ikiwemo Ujenzi wa Kituo cha Habari na mawasiliano Kwa nchi za afrika. na Ujenzi wa hosteli.
Alisema chuo kinatoa pia mafunzo ya kuongeza kazi za ubunifu ikiwemo banki,utalii na bima ambapo Vijana wengi wamewezeshwa na kujiajiri Kwa kuanzisha kampuni zao za kutengeneza sabuni na bidhaa zingine.
lengo la chuo Katika kipindi cha miaka kati ya mitatu hadi minne ni kuwa na Wahadhiri wenye PHD kati ya 30 hadi 40.
Mwisho .