Na Mwandishi wa A24Tv
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati Dkt.Dotto Biteko amesema Mtu asiyejifanyia Tathmini atakuwa mtu wa kuduwaa wakati wote au mtu asiyejifanyia tathmini atakuwa mtu wa kushangaa tu au kushangaza wengine…. nnachataka kusema ni kwamba serikali kama haitafanya tathmini ya shughuli zake haitapata uwezo wa kujipima imefanikiwa au imekwama wapi.
Aidha haitagundua vihatarishi vya utekelezaji wa mipango yake na ndio maana mh.Rais kama mnavyomsikiliza Moja ya jambo analolizungumza kwa nguvu zote na ambalo anatupa Kazi ya kulifanya ni sisi serikali kuwa na uratibu wa shughuli zetu tunazozifanya.
Kwa mujibu wa Dkt.Biteko serikali yetu imegawanyika maeneo mengi ipo serikali kuu na serikali za mitaa lakini unaweza kukuta serikali wakati Fulani kila Moja anafanya jambo lake na mwisho wa siku hakuna mifumo inasomana tujifanyie tathmini ili mwisho wa siku tusije kuwa watu wa kuduwaa na kujiuliza hili limetokeaje.
Alisema kuwa viongozi wote wanatakiwa kufuata miongozo hiyo katika utendaji wao wa majukumu ya serikali ili kusaidia kuongeza utoaji huduma Bora kwa wananchi, kwani viongozi wakuu wanaimani na Kongamano hilo kusaidia uboreshaji wa huduma za shughuli nzima za serikali.
Hata hivyo Dkt.Biteko amesema Ufuatiliaji wa masuala ya serikali ni muhimu kuwepo katika kuongeza tija ufanisi kwa sababu inaiwezesha taasisi kubaini changamoto na kuzifanyiakazi kwa wakati na hatimaye kutimiza malengo yaliokusudiwa na asitokee mtu kuhoji suala hilo.
Alisema pasipo na tathmini ni vigumu kufahamu mwendo wa utekelezaji wa mipango na mikakati ya serikali hata kama imeandaliwa kwa weledi wa hali ya juu ambapo asiyejifanyia suala la Ufuatiliaji atakuwa mtu wa hasara wakati wote nataka kuwahakikishia kwamba Kazi ya kujifuatilia wenyewe ni Kazi inatufanya kubaini matatizo mapema kabla hayajaleta hasara na tuyarekebishe mapema.
“kwa kuzingatia jukumu la kikatiba kama ilivyoainishwa katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara 52 kifungu cha 1 hadi 3 suala la usimamizi wa shughuli za serikali na kutokana na ukweli kwamba Kazi za usimamizi wa shughuli serikali haziwezi kufanikiwa kama hakuna mifumo mizuri ya Ufuatiliaji na tathmini juu ya shughuli zake”
“Nataka kutoa wito kwenu hasa kwa nyinyi mlio serikalini sisi tunadhana ya kuamini ili ifanyike jambo lolote lazima kwanza kuwe na rasilimali fedha halafu ndio jambo hilo lifanyike kama hatufikirii kuanza kufanya kabla rasilimali fedha hata tukipewa fedha hatutakuwa na matokeo, hivyo hili jambo la Ufuatiliaji na tathmini ni la kwetu wote kila taaluma lazima tujifunze kujitathmini”
Aidha Serikali imefanya maboresho ya kimuundo katika ofisi ya Waziri Mkuu sera bunge na uratibu na kuanzisha idara maalumu ya tathmini na ufuatilia wa shughuli za serikali Lengo likiwa ni kuimarisha shughuli hizo katika utekelezaji wa mipango program na miradi mbalimbali inayotekelezwa hapa nchini.
Alisema Lengo kuu la kupima utendaji wa shughuli za serikali ni kuhakikisha mipango mbali mbali ikiwemo dira ya taifa ya maendeleo na mpango wa taifa wa maendeleo Ilani ya uchaguzi na mipango mbalimbali mingine zinafikiwa kwa malengo yaliotarajiwa
Alisema kuwa katika kuimarisha suala Zima la Ufuatiliaji wa shughuli za serikali imeendelea kuchukuwa hatua mbalimbali zifuatazo mosi kuboresha muundo wa ofisi na kuanzisha idara mahususi ya tathmini na ufuatiliaji ikiwa ni pamoja na kuazisha idara hizo katika maeneo yote ya wizara
Kwa Upande wake Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Jinista Mhagama amesema wanaimarisha ushirikiano kwa kufanya Kazi kwa pamoja na wadau mbalimbali katika kujenga uwezo eneo la Ufuatiliaji na tathmini na hasa matumizi ya matokeo ya tathmini katika kuimarisha mwendo mzima wa utendaji serikalini na utoaji wa huduma bora kwa wananchi wa Tanzania.
Alisema kwamba Kongamano hilo linajumuisha kama nilivyosema awali makatibu wakuu, mabalozi makatibu tawala mikoa wakurugenzi wa Ufuatiliaji na tathmini sanjari na wataalamu wabobezi ndani na nje Tanzania katika dhana ya Ufuatiliaji na tathmini lakini vilevile na wizara na idara zinazojitegemea SMT na SMZ na wadau kutoka sekta binafsi na kimataifa.
Mwisho…….