Site icon A24TV News

EWURA KANDA YA KASKAZINI YAENDESHA KIKAO KAZI NA WAMILIKI WA VITUO VYA MAFUTA

Na Geofrey Stephen Arusha

Katika kupunguza tatizo la upatikanaji wa mafuta kwa wafanyabiashara binafsi wanaouza mafuta (petroli) ambalo linawapelekea mafuta kukosekana katika vituo vyao na wananchi kuteseka ,

wafanyabiashara kanda ya kazskani  wametakiwa kuingia mikataba na wafanyabiashara wakubwa wanaoagiza mafuta nje ili wawe na uhakika wa upatikanaji wa mafuta na kuondoka shida ya kukosekana mafuta katika vituo vyao.

Hayo yamebainishwa na meneja wa kanda ya kaskazini wa mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji (EWURA)Lorivii Lon’gidu wakati akiongea na wafanyabiashara binafsi wa mafuta katika kikao kazi kilichoandaliwa na EWURA kikiwa na lengo la kukumbushana taratibu za ufanyaji biashara ya uhuzaji wa mafuta kikao.

kilichowashirikisha wafanyabiashara wa mikoa ya kanda ya kaskazini ikiwemo Arusha, Kilimanjaro na Tanga.

Amesema kuwa kikao hicho kimeandaliwa kwa ajili ya kuweza kuwakumbusha wafanyabiashara hao wajibu wao wa kuwauzia wananchi mafuta bila kubagua na kufuata taratibu na sheria  kunabaadhi ya wafanyabiashara wamekuwa hawafati taratibu na sheria za ufanyaji wa biashara ya mafuta .

“Ila pia tumewataka wafanyabiashara hawa kuwa na mikataba na waagizaji mafuta lengo la mikataba hii nini nini ?wanakuwa na uhakika wa upatikanaji wa mafuta ,sababu hawa waagizaji mafuta wakubwa wanatabia moja unapo agiza mafuta lazima wajue hayo mafuta wanamuuzia nani ,kunaambao wanamikataba na sisi tunayo ilituweze kufatili lakini kunaambao hawana mikataba na wengi wao ndio wanakosa mafuta na kuanza kulalamika ”

lengo la mikataba hii nikuhakikisha kwamba bidhaa ya mafuta inapoagizwa ,hawa wafanyabiashara wakubwa kujua wanakwenda kuwauzia wafanyabiashara binafsi Kwa utaratibu gani ,ili huduma ya mafuta iweze kuwafikia wananchi Kwa wakati na maeneo ya mbali zaidi.

Kwa upande wao wafanyabiashara binafsi waliouthuria kikao hicho walisema kuwa kunabaadhi yao wanamikataba na wafanyabiashara hao wakubwa lakini wekuwa wakikosa huduma ya mafuta ,huku wengine wakizungushwa kupata mafuta hayo na wengine wakiambiwa walipe fedha mara mbili.

“Unakuta mimi nimelipia mafuta leo kwa uyo mfanyabiashara mkubwa nanina mkataba lakini cha kushangaza nikitaka mafuta nazungushwa muda mungine naambiwa niongezee fedha mafuta yamepanda lazivyo nirudishiwe fedha au unakuta kunamtu anataka nitoe cha juu ili nipate ukiangalia kituo changu cha mafuta akina mafuta ,mkuu wa mkoa anakuja anajua nimeficha mafuta ,toyo ambazo ndio wateja wetu wakubwa wanakuja wanataka kunitoa roho “alisema Maico masanja mfanyabiashara binafsi kutoka Tanga

Waliomba serikali kukaa na wafanyabiashara wakubwa wanaoagiza mafuta kupanga bei ambayo itakuwa hamnyimi faida muagizaji na ambayo haita muumiza mwananchi kwani Kwa sasa ivi bei iliopangwa inamuumiza muagizaji na ndio maana baadhi yao hawauzi mafuta kwa wafanyabiashara ambao ni binafsi Kwa kukwepa hasara.

Mwisho