Na Geofrey Stephen Arusha .
Mkoa wa Geita umetajwa kuwa kinara wa uzalishaji wa Madini ya dhahabu yanayochimbwa maeneo mbalimbali katika mikoa ya kimadini ambayo Madini mkoa wa Geita na Madini Mbogwe ikilinganishwa na mikoa mingine.
Hayo yamesemwa Septemba 26, 2023 na Kaimu Mkuu wa Geita Grace Kingalame ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale wakati akihairisha semina kuhusu fursa za kijamii na kiuchumi zinazopatikana mkoani Geita.
Akizungumza kuhusu shughuli za Madini zinazofanyika katika Mkoa wa Geita , Kingalame alisema shughuli za Madini zimegawanyika katika makundi manne ambayo ni Utafiti wa Madini, Uchimbaji, Uchenjuaji na uuzaji yaani biashara za Madini.
Mkoa wa Geita kwasasa una leseni mbalimbali zikiwemo leseni kubwa 2 za uchimbaji, leseni za utafiti 127, leseni za uchimbaji mdogo 803, uchimbaji wa kati 8 , leseni za biashara kubwa (Dealers) 47 na biashara ndogo (Brokers) leseni 33, leseni za uchakataji 33 na mitambo ya kuchenjulia madini leseni 265.
Takwimu za uzalishaji wa dhahabu kutoka Tume ya Madini mkoani Geita zinaonesha kuanzia mwaka 2017 mpaka 2023 kiasi cha kilogram 111,585.56 zimezalishwa.
Kwa kipindi cha miaka saba mwenendo wa uzalishaji wa madini ya dhahabu ulikuwa kama ifuatavyo mwaka 2017/18 kiasi cha kilogram 18,483, 2018/19 20,008 kg, 2019/20 14,251.65 kg , 2020/21 23,931.33 kg.
Aidha, mwaka 2021/2022 kiasi cha kilogram 16,274.12 zilizalishwa na mwaka 2022 /23 kilogram 18,585.56 zilizalishwa.
Mkoa wa Geita una migodi mikubwa miwili ambayo ni Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) na Mgodi wa Buckreef .
Mkoa wa Geita una wilaya tano ambazo ni Wilaya ya Geita , Bukombe, Mbogwe, Nyang’wale na Chato.
Mwisho .