Site icon A24TV News

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE LA BAJETI YARIDHISHWA NA TAEC TUTAJADILI CHANGAMOTO ZAO

Na Mwandishi wa A24Tv ,Arusha .

Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) Kanda ya kaskazini kudhibiti matumizi salama ya vyanzo vya mionzi vinavyo patikana katika mboga za majani ambazo hulimwa katika sehemu zenye madini ya urani ambayo humpelekea mtumiaji kupata madhara  kwa upimaji udongo huku ikitajwa kuwa madhara hayotokani na viuatilifu wanavyo tumia kulimia mazao.

Wakizungumza katika ziara ya kamati ya kudumu ya bunge ya bajeti ilipotembelea ofisi za tume ya nguvu za atomu Tanzania [TAEC] Kanda ya kaskazini Peter Pantaleo  ambaye ni mtaalamu wa mazingira .

Amesema kwenye mazingira ya kawaida kuna mionzi ambayo inatokana na madini ya urani ambayo hufyonza madini yanayotoa mionzi na kuhifadhiwa katika mazao.

Naye  DENIS MWALONGO ambae ni mtafiti amesema mionzi hiyo ni hatari katika chakula kwani kiwango kidogo kinaweza kuua watu wengi bila wao kujijua kilicho waua.

Kwa upande wake Daniel Sillo  ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya bajeti amesema TAEC kanda ya kaskazini wanafanya kazi ya kizalendo kwa kutetea usalama wa nchi na wananchi.

Naye Prof Lazaro Busagala ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa nguvu za Atomu Tanzania,amesema serikali imeendelea kuwekeza katika taasisi hiyo mpaka sasa imekwisha wekeza zaidi ya bilion ishirini na tisa na kumekuwa na ongezeko la maduhuli baada ya kuweka mfumo sahihi.

Aidha aliomba serikali kuongeza bajeti zaidi kwa ajili ya kutatua  changamoto  mbalimbali za kibajeti katika rasilimali watu ,vifaa na fedha kwa ajili ya kuendeshea  kituo hicho huku akiwataka kuendelea kusimamia vizuri zaidi .

Mwisho.